02.12.2018: SHILO 2018: PICHA ZA PAMOJA ZA WAZEE WA KANISANI, WACHUNGAJI NA WAGENI KATIKA KONGAMANO LA SHILO TANZANIA 2018
Katika uzinduzi wa kongamano la Shilo Tanzania siku ya Jumapili 02.12.2018 uliofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni wachungaji kutoka makanisa ya Mlima wa Moto Tanzania, wazee wa kanisa la MLima wa Moto Mikocheni "B", watumishi wa Mungu mbalimbali kutoka makanisa mbalimbali waliweza kupiga picha ya kumbukumbu na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ofisini kwake baada ya ibada kumalizika.
Kumbuka kongamano la Shilo hufanyika mara moja tu kwa mwaka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na huwakusanya watu kutoka kila pande ya dunia. Kwa mwaka huu kongamano hili lilizinduliwa Jumapili 02 na kuhitimishwa Jumapili 09/12/2018. Bishop Dr. Dunstan Maboya ndiye aliyezindua kongamano akishirikiana na mwenyeji wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Kongamano lilikuwa ni la siku 8 za Moto Usiozimika. Kulikuwa na wanenaji kutoka Kenya kama vile Rev. Dr. Lucy Natasha, Pastor Paul Kuria, Pastor Mahina na Tanzania kulikuwa na Bishop Dunstan Maboya, Mch. Sylvanus Komba kutoka Dodoma, Mch. Godfrey Fungo kutoka Mwanza na wachungaji wote wa makanisa ya Mlima wa Moto Tanzania

Comments
Post a Comment