06.05.2018: MAOMBI YA KUOMBEA MATUNDA KWAAJILI YA KUPATA MAONGEZEKO KATIKA MAISHA YA WATU YAFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"
Matukio katika picha ya ibada ya KUKOMESA UTASA NA KUKARIBISHA MAONGEZEKO katika maisha ya watu. Ibada hii ilifanyika siku ya Jumapili 06.05.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada hii iliambatana na maombi maalum kwaajili ya kuyaombea matunda ambapo kila mtu aliweza kuja na tunda lake kanisani. Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo waliweza kuyaombea matunda hayo na kuyabariki. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alisema, mtu akila tunda hilo lililoombewa na akiamini nguvu za Mungu zilizomo katika tunda hilo , basi ataanza kuona milango ya mafanikio ikifunguka. Tunatambua kuwa watu wengi wamefungwa katika biashara zao, kazi zao, uzao wao, afya zao na mengine kama hayo, kwahiyo kupitia maombi haya ya vitendo, Mungu atakwenda kuwafungua na Jumapili wataleta shuhuda zao katika hekalu la Mungu.
Katika Biblia tunasoma ya kwamba Yesu alitumia mate na tope kumponya kipofu, Paulo na Sila walitumia nyimbo zao na milango ya gereza ikafunguka na wakawekwa huru, Munsa alitumia fimbo kuigawa bahari na watu wakapita katikati ya bahari, nasi leo tunatumia matunda na kwa wale wenye imani ya kweli ya kumwamini Mungu kwa zile nguvu alizoziweka katika matunda hayo.
Wewe uliyekosa ibada ya Jumapili tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Kanisa limekuandalia usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3
Bishop Mhe. Gertrude Rwakatare (kushoto) akigawa matunda kwa waumini
Mch. Stanley Nnko
Mch. Mainah
Mch. Stanley Nnko
Comments
Post a Comment