Watangazaji wa Praise Power Radio - Hudson Kamoga sambamba na Veronica Frank
Veronica na Hudson wakimtambulisha James
Boniface Magupa, George Mpella na watu mbalimbali wakiwa makini kabisa
Joyce Charles, Lista, Tina Mtua, James, George Mpella, Magupa wakiwa wametulia katika uwepo wa Bwana
mamia ya watu wakiongozwa sala ya toba
Watu wakifunguliwa kutoka katika vifungo vya ibilisi
KESHA
KILA IJUMAA YA MWISHO WA MWEZI NA PRAISE POWER RADIO
HAKIKA
NI ZAIDI YA MKESHA
Maelfu ya watu wamekuwa
wakihudhuria mkesha huo wa Ijumaa ya kila mwisho wa mwezi. Ni mkesha unaoandaliwa
na kituo cha Praise power Radio wakishirikiana na kanisa la Mlima wa moto.
Ni
mkesha uliojaa matendo makuu ya Mungu, shuhuda zinazogusa mioyo ya watu pamoja
na kipindi cha sifa ambapo kwaya, vikundi mbalimbali pamoja na waimbaji binafsi
huongoza sifa.
Pia
kikundi kipya cha sifa kinachoongozwa na mwalimu John Shabani, kimekuwa gumzo
katika mikesha hiyo. Kikundi hicho kinachoendelea kujifua kila wiki ndani ya
kanisa la mlima wa moto, kimeendelea kupongezwa kwa kufanya vizuri.
Ijumaa
hii, imekuwa ni ijumaa ya kipekee; tumeshuhudia mamia ya watu wakimpokea Bwana YESU. Pamoja na
shuhuda mbalimbali, lakini ushuhuda wa kijana JAMES, kijana aliye ibuliwa na
kipindi cha Rise and Shine cha Praise Power radio; umekuwa ni ushuhuda wa
kipekee. James ni kijana aliyetupwa na mama yake mzazi akiwa mototo mchanga.
Aliokotwa akiwa ndani ya box huku mbwa wakigombea box hilo. Mpaka sasa James,
yeye ndiye baba, yeye ndiye mama nay eye ndiye ukoo. Lakini uongozi wa Praise
power Radio na Mlima wa moto wameamua kusimama na James. Ni kijana ambaye bado
anahitaji msaada wa kibinadamu; hivyo hata wewe waweza ukatoa chochote kwa
ajili ya maisha ya James.
Watu
wa aina mbalimbali wamekuwa gumzo katika mkesha huo. Hatuwezi kuwataji wote,
lakini hawa ni wachache tu:
Amefafanua mambo mengi likiwepo
la kanisa kujikita na kutumia zaidi
mitandao ya kijamii ambayo mambo mengi yanayoonekana humo ni ya kukipotosha kizazi chetu. Mitandao hiyo ni
kama: Facebook, Blogs, Websites, Whatsup, Youtube, Twitter, Skype na kadhalika.
Kipindi chake cha kuijua
sheria kinachoendeshwa na Rise and Shine ya Praise power Radio, kimewasaidia
watanzania wengi kujua sheria ya nchi, sheria ya kimataifa na haki za kila
mmoja.
Hakika, wazo hili la kuwa na
mkesha unaowakutanisha watu wa dini zote na madhehebu yote, watu wa rika zote
na makabila yote; ni wazo la kupongezwa na kutiwa moyo.
Pongezi siwafikie Uongozi wa
Praise powe radio (George Mpela, Igokolo, Hudson Kamoga, Veronika Frenk, Tina
Mtua, Victor Aron, Joyce Charles, John Kisaka, Erick Briton, Frida Kimambo
Mtue, Joseph Handrick, Mama Martha, mzee kibona, Lista n.k)
Uongozi wa Mlima wa Moto
chini mbeba maono na mchungaji kiongozi wa Mlima wa moto, Dr. Getrude Pangalile
Rwakatare.
Comments
Post a Comment