27.01.2019: YONA AMVISHA PETE YA UCHUMBA MCHUMBA WAKE GERTRUDE SHINDA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Katika ibada ya KUZIOMBEA FAMILIA ZETU iliyofanyika siku ya Jumapili 27.01.2019 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikoceheni "B", mtumishi wa Mungu Yoha Mwakamala alimvisha pete ya uchumba mchumba wake Gertrude Shinda.

Yawezekana na wewe unatamani kupata mtu wa kukuoa au mtu wa kumuona lakini umejitahidi kumtafuta imeshindikana. Pengine ulimchumbia lakini uchumba wenu ukaharibika kabla ya kufikia hatua ya kuvishana pete.
Leo nataka nikutangazie ya kwamba yupo Yesu Mtenda miujiza katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kila aliyefika hapa na kujiunga na kanisa hili Mungu aliweza kufungua milango ya mafanikio katika mambo mengi na hasa wale wanaohitaji kuoa na kuolewa.


Unapojiunga na kanisa hili na kujitamkia kuwa utamtumikia Mungu kwa uaminifu, basi Naye BWANA anafungua milango ya mafanikio katika maisha yako. Wapo watu wengi sana wamekuwa wakitafuta watu wa kuwaoa au kuolewa nao lakini walipofika katika kanisa hili Mungu aliweza kuwapa waume zao na wake zao na sasa wanafurahia maisha yao ya ndoa.


Sio mpango wa Mungu wa wewe kuishi maisha ya ubachela, maisha ya upweke. Yawezekana kuna watu wamekunenea maneno mabaya ili usiolewe au usioe. Mungu ni mwaminifu na ni mwema anaweza kukupa yule umpendaye kama utamkubali na kumtumikia.

Nikualike katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada yetu itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana





































Comments