28.10.2018: MATUKIO KATIKA PICHA YA WATU WAKITOKWA NA MAPEPO KATIKA IBADA YA MAOMBI HATARI

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya katika kanisa la Mlima wa Moto MIkocheni "B" kila itwapo leo.
Siku ya Jumapili 28.10.2018 katika ibada ya "MAOMBI YA HATARI" iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto MIkocheni "B" tulishuhudia watu wakifunguliwa kutoka katika mikono ya shetani na kuwekwa huru. 



Nikishirikiana na wachungaji, wainjilisti na waumini tuliweza kufanya maombi ya hatari ya kuangamiza kila kazi za shetani ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma watoto wa Mungu wasifikie pale wanapotaka kufika. Wakati wa maombi watu walitokwa na mapepo, majini, nguvu za giza ambazo zimekuwa zikiwatesa kwa kipindi kirefu sana. Hakika Mungu wetu anafanya mambo ya ajabu na ndio maana hatuachi kumtumikia kila kuitwapo leo. 


Wakati tukiwaombea watu tulishuhudia mapepo yakipiga kelele yakitaka kuondoka kwasababu yalikuwa yakiuunguzwa na moto wa Mungu. Watu walikuwa wakigalagala chini, wakihangaika kwasababu damu ya Yesu ilikuwa ikifanya kazi ndani yao, ikisafisha kila uchafu uliowekwa na ibilisi.


Yawezekana unateseka na mapepo, majini, nguvu za giza ambazo zimesababisha usioe/kuolewa, mimba kuharibika, usipate kibali, usiinuliwe, usisafiri, usipate wateja, pesa zikija zinatumika katika matumizi ambayo hukuyapangilia, magonjwa sugu, ajali za mara kwa mara, vidonda sugu, kuota ndoto mbaya, kufeli masomo, kupotelewa na ndugu, vifo visivyo vya lazima, kila amayekuona anakuona kama hufai, kutokubalika katika jamii yako, roho za kukata tamaa, roho ya kujiua, kushindwa kusoma Neno la Mungu, kukosa hamu ya kuja kanisani, roho za usinzi, umalaya, uasherati, ushoga, ulimbukeni, kutowatii watumishi wa Mungu, usengenyaji, kulipiza kisasi kwa mabaya, roho ya wivu, tamaa na mambo mengine mabaya kama hayo. BWANA anaweza kuyaondoa haya yote kama utafika hapa kanisani na kuwatii watumishi wa Mungu kwa yale ambayo utakuwa ukielekezwa baada ya maombi kufanyika, Pia kama utakuwa na ile iMANI ya kweli kwa kila kitu utakachokuwa ukifanyiwa na watumishi wa Mungu. 


Ninakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Tutakuombea na BWANA atakuweka huru kabisa. Njoo ukiamini ya kuwa UTAFUNGULIWA katika jumba lako la mateso na shida.


Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3


----------
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Ibada ya Jumapili 28.10.2018
Ibada ya Maombi Ya Hatari.



















Comments