28.10.2018 | MARY AJIONA AKITOKA KWENYE JENEZA NA WANAE

Mary alikuwa ni muumini mzuri wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kipindi cha nyuma lakini baadae akaamua kuacha kuhudhuria ibada zetu na akaendele na maisha yake ya kawaida huko mitaani. Baada ya changamoto za kimaisha aliamua kanisani na kumtumikia Mungu. Siku ya Jumapili 28.10.2018 katika ibada ya Maombi ya Hatari iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kufika na kuhudhuria ibada hiyo. Akiwa kanisani wakati maombi yanaendelea aliweza kuona jeneza likimwaga wanae na yeye akiwemo ndani ya jeneza. Mary alikuwa na haya ya kushuhudia.


BWANA Yesu asifiwe. Kwa jina naitwa Mary, nimekuwa nikihudhuria ibada za Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa kipindi kirefu lakini hapa katikati sijui ni kitu kiliniingilia nikawa siji kanisani. Siku ya leo ya Jumapili ya 28.10.2018 nilipofika katika kanisa hili nimeona jeneza linafunguka juu kwenye paa na watoto wanatoka na mimi ninatoka kwenye jeneza yaani jeneza lilikuwa linatumwaga chini mimi na watoto wangu.

Mungu wetu ni waajabu sana, kumbe mimi nilikuwa kwenye jeneza na wanangu bila ya kujua. Ninamshukuru sana Mungu kwa kutupa mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, amekuwa msaada katika familia yetu kupitia maombi yake. Kitendo cha kuona wanangu wanatoka kwenye jeneza ni tukio kubwa sana katika maisha yangu, ninaami sasa tumetoka katika jeneza la mateso na nitazidi kumtumikia Mungu katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni “B” pamoja na watoto wanangu. Asante sana.

BONYEZA HAPA KUONA VIDEO YAKE: https://www.youtube.com/watch?v=1Ugw007mpIk





Comments