28.10.2018: BAADA KUANGUKA GHAFLA APATA UGONJWA UNAOMTESA MPAKA SASA


Mama mmoja aliweza kufika katika ibada ya maombi ya Hatari iliyofanyika siku ya Jumapili 28.10.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” akihitaji watumishi wa Mungu wamuombee mgonjwa wake. Akiwa katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” alikuwa na haya ya kusema, 

BWANA apewe sifa. Huyu mgonjwa wangu mwezi wa tatu (3) mwaka 2018 alianguka ghafla na baada ya kuanguka aliweza kupata ugonjwa huu unaomtesa mpaka leo.na ugonjwa huo ni “stroke”. Tumehangaika sana bila ya kupata majibu, lakini tuliposikia habari za kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kuwa Mungu anaponya magonjwa sugu tuliweza kuja mara moja kwaajili ya uponyaji.

Baada ya kumaliza kuongea, wachungaji waliingia vitani kuvunja kila roho chafu, mapepo, majini, vinyamkela na kila nguvu za giza zilizosababisha huyu mzee kupata ugonjwa mbaya wa “stroke”. Kama watu wa Mungu naomba tuungane kumuombea huyu ndugu yetu ili BWANA aweze kuponya na aendelee na shughuli zake za kila siku.


Comments