11.11.2018: MKE WA DAMAS KOMBA NA MUME WAKE WAMSHUKURU MUNGU KWA JARIBU ALILOPATA KATIKA FAMILIA YAKE

Kuna wakati mtu unapitia magumu lakini Mungu mwenye huruma huingillia kati na kututia nguvu. Kuna kipindi unakuwa na mawazo mengi ni jinsi gani unaweza kulipita jaribu lako lakini Mungu huingilia kati na kutuvusha salama katika majaribu. Mungu ni mwenye huruma sana  hasa kwa yule anayemtumikia na kumtegemea kwa kila kitu. 


Siku ya Jumapili 11.11.2018 katika ibada ya KUFUNGULIWA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" watumishi wa Mungu Damas Komba na mke wake waliweza kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoyafanya katika jaribu walilolipata katika familia yake hasa upande wa mke wa Damas Komba. Ilikuwa ni wakati mgumu sana kwao lakini BWANA aliweza kusimama upande wao na kuwafuta machozi na sasa wanaendelea na kazi ya Mungu.
Wakiwa katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" walimshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea katika familia yao, walimshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, wachungaji, wazee wa kanisa, wainjilisti, viongozi wa idara, wahudumu , vijana na waumini wote kwa maombi yao na ushirikiano walioonyesha katika kipindi chote walichokuwa wakipitia. Pia shemeji yake na Damas Komba alishangazwa na jinsi wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" walivyokuwa mstari wa mbele kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa wakati wa mapito yao.
Kama kanisa tuzidi kuwaombea watumishi wa Mungu hawa ili wazidi kusonga mbele kumtumikia Mungu. Tuwaombee dhidi ya maadui zao, tuwaombee wakafanikiwe kimwili na kiroho, tukawaombee wakainuliwe kila mahali. Mungu akasimame upande wao hasa katika huduma waliyo nayo ya kuwaleta watu kwa Yesu Kristo. Watumishi hawa wamefanyika nguzo katika kanisa letu, wamefanyika baraka kwa kila mtu kutokana na mchango wao mkubwa wa kuwainua watu kiroho na kimwili.  katika maombi yetu ya kila siku tuwakumbuke na kuwaomba ili uwepo wa Mungu na neema za Mungu ziwe juu yao katika maisha yao yote.
Yawezekana ulikosa kuwafariji katika kipindi cha mapito yao au siku ya Jumapili iliyopita, basi tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana ili uweze kuwatia moyo na kujua ni changamoto gani walikuwa wanapitia.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3























Comments