04.11.2018: SANDUKU LA MAOMBI KIPINDI CHA KONGAMANO LA SHILO 2018 LAZINDULIWA RASMI NA KUOMBEWA.

Sanduku la maombi ambalo huandaliwa katika kipindi cha kongamano kubwa la Shilo 2018 liliweza kuzinduliwa rasmi na kuombewa na watumishi wa Mungu ili kila atakayeweka maombi yake yaweze kupokelewa na Mungu. Maombi yote waliyoandika waumini yataweza kuombewa na wachungaji, wainjilisti, wanamaombi ili Mungu aweze kutimiza ndoto zao


Shilo ni Kongamano kubwa ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka katika kanisa la Mlima waMoto Mikocheni "B" na hukusanya makanisa yote ya Mlima wa Moto duniani, watu kutoka mataifa mbalimbali bila kujali dini, kabila, umaarufu, jinsia, rangi n.k. 

Watu wote hukusanyika pamoja kwa lengo moja la kumshukuru Mungu kufikia mwisho wa mwaka, na kumuomba Mungu atulinde na mwaka ujao, kupeleka maombi yake kwake ili ashughulike na maisha yetu, kumuomba Mungu atuinue kiroho na kimwili, kupata muda wa kutafakari matendo makuu ya Mungu aliyotutendea kwa mwaka mzima, kujifunza masomo mbalimbali yatakayosaidia kutangaza Habari Njema za Yesu, kufanya maombi ya vita na ya hatari dhidi ya wabaya wetu waliosababisha maisha yetu yasiwe na muelekeo mzuri, kuinuana kiimani, kutubu makosa yetu, kumkumbusha Mungu maombi yetu ya mwaka mzima, kupokea miujiza yetu kutoka kwa Mungu, kufunguliwa katika mikono ya wabaya wetu, kujazwa nguvu mpya, kumpokea Roho Mtakatifu, kukombolewa kutoka katika mitego ya shetani, kupokea uponya mkuu kutoka kwa Mungu na mambo mengine kama hayo.


Kwa mwaka huu kongamano la Shilo litaanza Desemba 02 hadi 09/2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Siku za Jumapili kongamano litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na siku za katikati ya wiki litakuwa likianza saa 9 alasiri kwa siku zote 8.


Kwahiyo tunakuomba sana uandike maombi yako na uweze kutumbukiza katika sanduku hili la maombi. Watumishi wa Mungu watayaombea maombi yako na BWANa atafanya jambo katika maisha yako kulingana na kile ulichokiomba. Mungu wetu wa mbinguni ni mwaminifu sana hasa kwa wale wamtegemeao na wanaofanya yale anayowaagiza kupitia watumishi wake na kupitia Biblia yake. Imani yako na jitihada zako za kufika katika hekalu la Mungu ndivyo vitakavyosababisha ukutane na muujiza wako, kwahiyo usipuuzie kabisa kuhudhuria kongamano hili la kihistoria.


Mwisho tunapenda kukushirikisha katika baraka hizi kwa kuchangia kufanikisha kongamano hili la Shilo kwa kutuma mchango wako wa pesa kwa Tigo Pesa 0677 045 504 na Mungu atakubariki sana na atabariki kazi ya mikono yako. Mchango wako ndio utasababisha kupata umeme, kuwasafirisha watumishi wa Mungu wanaotoka nje ya Tanzania na nje ya mikoa ya Dar es Salaam, malazi na chakula kwa watumishi wa Mungu, kuchangia nauli kwa waimbaji watakaokuja kwaajikli ya kazi ya Mungu, kulipia vifaa vya usafi wa kanisa na maeneo mbalimbali ili kulinda afya za watu, kulipia ulinzi wa mali za watu, kulipia bill za maji kwani kuna baadhi ya watu watakuwa wakilala kanisani wakimuomba Mungu, kununua vifaa vitakavyokuwa vikiharibika kipindi cha kongamano, kuwalipia nauli wale ambao watakuwa wameishiwa nauli za kufika majumbani mwao na gharama zingine mbalimbali za uendeshaji wa kongamano hili la Shilo. Tunakutegemea sana na Mungua atakubariki.


Ukituma pesa yako ambatanisha na maombi yako, nasi tutakuombea na Mungu atafanya njia pasipo na njia kwa damu ya Yesu. Mungu akubariki sana.


BONYEZA HAPA KUONA VIDEO YAKE: https://www.youtube.com/watch?v=e8GIEEufVv0





















Comments