04.11.2018: Mwimbaji wa Gospel Martha Baraka awachanganya waumini kanisani angalia tukio hili

MUNGU AZIDI KUMTUNZA NA KUMUINUA MARTHA BARAKA.

Ni maombi yangu Mungu azidi kumuinua mtumishi wa Mungu Martha Baraka (Woman of Faith) kwa huduma yake hii ya uimbaji. Mungu akampe mafunuo mapya yatakayosababisha watu wengi wakaja kwa Yesu kupitia uimbaji wake. Kitendo alichokifanya katika madhababu ya Mlima wa Moto Mikicheni "B" siku ya Jumapili 04.11.2018 hakitasahaulika kwamwe, maana alishusha uwepo wa Mungu kupitia karama yake hii ya uimbaji. Watu tulibarikiwa sana, tulijazwa nguvu mpya na mioyo yetu ilichangamka.




Tuzidi kumuombea huyu mtumishi wa Mungu ili kile kilichotegwa mbele yake na maadui zake juu ya huduma yake kikashindwe kwa jina la Yesu. Kila atakachokifanya kwa utukufu wa Mungu kikakubalike na kupokelewa kwa heshima, Mungu akafungue milango yake ya mafanikio ya kimwili na kiroho. 




Tuzidi kumuombea katika tamasha lake la uzinduzi wa albamu yake ya "FURAHA" itakayofanyika siku ya Jumapili 18.11.2018. Kama utahitaji kujua mengi kuhusu tamasha lake mpigie kwa namba hii +255 743 502 257 atakujulisha mengi..




BONYEZA HAPA KUONA VIDEO YAKE: https://www.youtube.com/watch?v=Cx_AmTM8NkE&t=49s




----------------------

Bishop Dr. Gertrude Rwakakatare.

Ibada ya Jumapili 04.11.2018

Ibada ya maombi ya Vita
















Comments