16.09.2018: WATU WAZIDI KUOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B


Unawe ukajidanganya na kusema, "Nitaokoka kesho, nitaokoka nikioa au kuolewa, nitaokoka nikijenga, nitaokoka nikinunua gari zuri, nitaokoka nikiwa na pesa nyingi, nitaokoka nikisafiri kwenda Ulaya, nitaokoka nikipata kazi, nitaokoka nikiwa tajiri". Unaweza kuwa na sababu nyingi sana za kusababisha wewe kuamua kuokoka,  lakini usijue lililo mbele yako. Maisha yetu yanaongozwa na Mungu na ndiye anayejua kesho yako au saa moja iliyo mbele yako. Unaweza kupanga yako na Mungu akapanga yake.



Kuokoka ni lazima kwa kila Mkristo. Unapookoka unajiunganisha na ufalme wa mbinguni, unajitenga na ulimwengu wa shetani, unafanyika kiumbe kipya, unaondolewa dhambi zako zote mara baada ya kutubu makosa yako, unaongozwa na Roho Mtakatifu, unafanyika mwanafunzi wa Yesu, unakuwa ni balozi wa Mungu hapa duniani, unahusika katika ufalme wa Mungu.

Lakini unapoacha wokovu, shetani anachukua nafasi yake na kukufanya mwananfunzi wake. Mungu anachukua kila kitu alichokiweka kwako wakati unaokoka na kukuacha  peke yako. Hii tumeshuhudia kwa watu wengi sana. Unamkuta mtu alikuwa ameokoka lakini baada ya kuacha wokovu maisha yake yanaanza kuwa mabaya na vituko katika maicho ya watu



Usijidanganye kuwa ukifanya jambo fulani ndipo utaokoka. Unaweza kupanga mambo mengi sana ya kufanya  na Mungu naye anapanga mambo mengi juu ya hatma ya maisha yako. Unaweza ukajikuta umri umeenda, matatizo yamekuvamia, magonjwa yamekuingia, maisha yamekupiga na bado unajidanganya ya kuwa ukifanikiwa ndipo utaokoka. OKOKA SASA UPATE MAFANIKIO ya kimwili na kiroho

Huu ni wakati wako mzuri wa kuokoka, hii ni nafasi yako ambayo Mungu amekupa ili uweze kuokoka. Unapookoka na kubatizwa kwa maji mengi ndipo Mungu naye anafungua milango ya mafanikio katika maisha yako. Unaanza kushangaa mambo yako yanakunyookea, kila unalofanya linakuwa jepesi

Maisha yetu ni mafupi kwahiyo tunahitaji kujiandaa kwaajili ya maisha yetu ya milele huko mbinguni na sio hapa duniani. Tunapaswa kuokoka, kubatizwa kwa maji mengi, kujazwa Roho Mtakatifu, kuongozwa na Mungu, kutenda yaliyo mema, kuachana na dhambi, kusoma Neno la Mungu, kufanya toba tunapomkosea Mungu, kutangaza Injili, kushiriki ibada katika nyumba ya BWANA, kuliishi Neno la Mungu, kuwaleta watu wengi kwa Yesu kwa kuwafundisha neno la Mungu na mambo mengine kama hayo.

Nichukue nafasi hii kuwapongeza waongofu wapya waliokoka katika ibada ya maombi ya "Kuvunja Roho ya Utasa la Laana" iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 16.09.2018. Maamuzi yao yatabadilisha historia ya maisha yao, imani yao itawaokoka katika shimo la shetani, kuthubutu kwao kutawaweka huru kutoka katika  nguvu za giza. Waongofu wapya  hawa wameongeza idadi ya wafuasi wa Mungu  na kupunguza idadi ya wafuasi wa shetani.

Tunakuomba wewe uliyeokoka uzidi kumtumikia Mungu, kushiriki ibada, kusoma Neno la Mungu, kutubu makosa yako unapoona umemkosea Mungu, kufanya maombi, kuwatii watumishi wa Mungu, kujitoa kwa kazi ya Mungu, ukatangaze Injili kwa mataifa yote, ukawalete watu wengi kwa Yesu, ukawe mtoaji wa zaka na sadaka kanisani, ukawapende watu wote bila ya kuchagua dini au taifa la mtu, ukaachane na dhambi n.k

Na wewe ambaye unatamani kuokoa, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3
























































Comments