02.09.2018: WALIOJIUNGA NA PRAISE & WORSHIP TEAM YA MLIMA WA MOTO MIKOCVHENI "B"




"Usipomuimbia Mungu basi Mungu anaweza kuinua hata mawe yakamuimbia. Usipomtumikia Mungu wapo wengine watakaomtumikia Mungu kwa viwango vya juu zaidi yako. Mungu hana hasara ila wewe ndio unayepata hasara kama humtumikii Mungu wako kwa mali zako ana akili zako."

Nikupongeze wewe mwanangu ambaye siku ya Jumapili 02.09.2018 kwenye ibada ya KUZAA MUUJIZA WAKO iliyofanyika katika nyumba ya BWANA ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kuchukua maamuzi ya Kujiunga na Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Maamuzi yako ni sahihi na yanaleta utukufu mbele za Mungu. Huduma unayoenda kuanza sasa ya kumuimbia Mungu itasababisha MIUJIZA katika maisha yako, italeta mafanikio katika maisha yako, itafungua milango iliyofungwa na maadui zako. Ninasema haya, kwasababu Mungu wetu hupenda sana sifa, anapenda kusifiwa, anapenda kuimbiwa na hukaa katikati ya sifa. 

Mtu unapomsifua hujisikia vizuri sana na hufanya kila awezolo kukupongeza kwa zawadi au kwa neno "asante." Kwahiyo wewe uliyeamua kumtumikia Mungu kwa njia ya sifa tegemea kupokea "Asante" kutoka kwa Mungu, tegemea "Zawadi" kutoka kwa Mungu. Zawadi yaweza kuwa yoyote ile na mara nyingi zawadi huja kwa "Surprise", kwahiyo tegemea "surprise" kutoka kwa Mungu.

Mimi nikutakie safari njema ya kumtumikia Mungu kwa njia ya sifa, Mungu akuongoze katika huduma yako ya uimbaji uliyoianza, Mungu akupe sauti nzuri yenye kumfurahisaha Mungu wetu na wanadamu, Mungu akupe upako wa kuwaokoa watu kupitia nyimbo zako, Mungu akupe uwezo mkubwa wa kutunga nyimbo nzuri.

Unapofanikiwa kihuduma nakuomba mwanangu usijiinue na kuanza kiburi. Mungu hapendi kuona unajiinua na kuwaona wenzako hawajui kuimba. Kwahiyo jishushe na Mungu atakuinua. Ubarikiwe mwanangu.

Mwisho napenda kukualika wewe unayesoma ujumbe huu katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3











Comments