02.09.2018: MAHUBIRI YA BISHOP MHE. DR. GERTRUDE RWAKATARE KUHUSU KUZAA MUUJIZA WAKO

MWEZI WA TISA NI MWEZI WA KUPOKEA MAJIBU YAKO ULIYOOMBA MWEZI WA NANE
Mwezi wa tisa ni mwezi wa KUZAA. Mwanamke akipata mimba na akikaa miezi nane, na ukifika mwezi wa tisa anaanza kujiandaa , anaanza kununua pampasi, vitu vya watoto n.k kwaajili ya mtoto. Huu ni mwanzo mwa mwezi wa tisa ambao ni mwezi wa KUZAA. Je, wewe ni mmojawapo wa wale walio tayari kuzaa majumba, magari, watoto, mafanikio, viwanja, kufungua huduma zao, kuwa karibu na Mungu, kumtumikia Mungu, kupata waume wa kuwaoa, kupata wake wa kuoa, kuimarisha ndoa na baraka tele? 
Mwezi wa tisa uwe ni mwezi wa MATUNDA kwako , uwe ni mwezi wa KUZAA.



Unakumbuka mwezi wa saba tulisema ni mwezi wa KUSULISULI, mwezi wa kuleta nyama, ni mwezi wa kuokota kwale, ni mwezi kupokea mahitaji yetu kutoka kwa BWANA,kupokea Baraka, afya njema n.k. Mwezi wa nane tukasema ni mwezi wa KUKUSANYA NGUVU kwa kufanya maombi na kumlingana Mungu kwaajili ya mwezi wa tisa. Mwezi wa tisa nikasema, “Kama hutapata MUUJIZA nishike gauni.” Na huu ndio mwezi wa tisa wa kushikwa gauni langu kwa wale ambao hawajatendewa muujiza, ni mwezi wa kunishtaki. Mwezi wa tisa ni mwezi wa KUPOKEA kwahiyo ni lazima MAJIBU yako ya JIBIWE na Mungu. Kaa ukitarajia kupokea MAJIBU yako kutoka kwa BWANA.


BADILISHA AINA YA MAOMBI YAKO
Maombi yako ni lazima yabadilike. Ninakuomba ubadilishe namna ya MAOMBI yako. Achana na yale maombi uliyoyazoea kila siku. Soma Yerermia 15.18. 


Ninaongea na mtu mwenye tatizo la kudumu maishani mwake, ninaongea na mtu mwenye ugonjwa wa kudumu maishani mwake, mtu mwenye adui wa kudumu maishani mwake. Ninakuomba sana ubadilishe aina ya maombi yako ili kuondokana changamoto za kudumu zinazokusumbua kwa kipindi krefu. Kama utabadilisha maombi yako na ukaachana na maombi uliyoyazoea tegemea mambo makubwa kutoka kwa Mungu dhidi ya vikwazo unavyopitia. Achana na maombi ya kukariri, annza kufanya maombi ya kumaanisha mbele za Mungu. Omba huku ukiwa umejiachia kwa Mungu. tafuta eneo sahihi na muda sahihi wa kuongea na Mungu wako. Acha kuwa na maombi ya vuguvugu. Mungu atusaidie.


MAADUI WA KUDUMU NI LAZIMA TUWAKOMESHE
Katika maisha yetu haya tunaweza kuwa na maadui wa kudumu ambao kila kukicha wanapanga ni jinsi gani ya kukuharibia maisha yako. Maadui hawa wapo kwaajili ya kuharibu malengo ya watu. 

Adui anaweza kuwa mwananfamilia, rafiki yako, mfanyakazi wako, muumini mwenzako, mtu wako wa karibu n.k na wamekuwa ni msumari na mwimba katika maisha yako. Kila unachokifanya kizuri kwao ni kibaya, kila unapojitahidi kujikwamua kimaisha wao wanajipanga kukuharibia kabisa.

Sasa kama mtoto wa Mungu unatakiwa kukaa sawa katika maombi yako, unatakiwa kujipanga kupigana na hawa maadui zako kwa maombi. Nguvu ya Mungu ikiwa juu yako hakuna baya kutoka kwa adui yako litakalofanyika katika maisha yako. Sasa unatakiwa kujiuliza, "Je.unaingiaje kama mtakatifu wa BWANA kupambana na maadui zako? Unatakiwa kubadilisha “style” ya maombi ambayo umekuwa ukiomba na huoni majibu yako. Yawezekana maombi yako ni kukariri, unachokiomba hukimaanishi, unachokiomba hakina “connection” na Mungu wako. Maombi yako hayamgusi Mungu wako, maombi yako ni ya kawaida sana, maombi yako hayana kishawishi kwa Mungu wako. Kwahiyo unapoomba ni lazima umaanishe, ujitakase kwanza, utumie vifungu vya Biblia, uisome Biblia na kujua ahadi za Mungu juu ya maisha yako, maisha yako yawe ya kumpendeza Mungu, usiwe mnafiki katika maombi yaani wewe mwenyewe ni adui au ni mwiba kwa wenzako halafu unataka Mungu akuondoa kwa wale wanakuonea..Mungu atusaidie.

YAWEZEKANA UKAFUNGA NA KUOMBA LAKINI SHIDA ZIKABAKI PALEPALE KUTOKANA NA TABIA YAKO NA AINA YA MAOMBI YAKO UNAYOYAOMBA
Unaweza ukawa umefunga na kuomba na baadae ukaanza kulalamika mbona jeraha langu bado ni la kudumu, mateso yangu yamening’ang’ania, naona mpenyo hamna, naona hakuna njia.? Kila jambo unalolifanya halifanikiwi, malengo yako hayatimii, mipango yako haiendi sawa. Unaanza kumlaumu Mungu "Je, Mungu unaona au huoni, mbona shida zangu haziishi, kila ninalofanya kwangu ni zero, jitihada zangu hazileti matunda, mbona shida kwangu ni kama maji ya kijito ambayo husukuma kila kitu katika barabara yake? 

Unabaki kumlaamu Mungu wakati makosa ni yako mwenyewe. tatizo ulilonalo ni aina ya maombi unayoomba, style unayotumia kuomba jambo kwa Mungu wako sio sahihi, matendo yako hayampendezi Mungu, maisha yako sio mfano mzuri kwa Mungu wetu, tabia yako ni kama watu wa kidunia wasiomjua Mungu, maombi yako ni kukariri na sio ya kumaanisha, kufanya toba mbele za Mungu ni kama kituo cha polisi. Kwahiyo ili ujibiwe na Mungu unapaswa kutenda matendo mema, kuachana na dhambi, kufanya toba, kushiriki ibada, kusoma Neno la Mungu na kuliishi, kuwa na upendo kwa kila mtu, kufunga na kuomba kwa kumaanisha na sio kufanya maombi ya klulazimishwa na kiongozi wako, fanya maombi ya hiari kutoka ndani ya moyo wako, tengeneza mazingira maalum na muda maalum ukiwa umetuliza akili yako wakati wa kuomba n.k. Ukifanya hayo yote, Mungu lazima aonekane katika maisha yako. 

Mungu anaweza kuonekana kwetu kutokana na matendo yetu mema na uweza wake na nguvu zake zitakuwa juu yetu. Mungu anapokuwa ndani yetu ndipo tunapojiona kuwa sisi tuko tofauti na watu wa dunia, pia tunapoona Mungu akiingilia kati shida zetu za kudumu ndipo tunapotambua kuwa Mungu wetu yuko nasi. Inapendeza sana unapoona Mungu akijibu maombi yako kwa wakati. Unaweza kujibiwa na Mungu kama utakuwa ukiyatekeleza yale anayokuagiza katika kitabu chake kitakatifu yaani Biblia na kuyafanya yale wanakuagiza watumishi wake madhabahuni. Mungu atusaidie sana!


JE, UNASHIDA AMBAYO IMEKUG’ANG’ANIA?
Je, una tatizo la kudumu? Unaugonjwa ambao hutaki ukuachie? Umekwama kwa namna moja au nyingine kwasababu ya mtu tu, unajitahidi kufanya kazi lakini umekwamishwa, . Kuna watu wanakwamisha wenzao wasiendelee mbele, kuna watu waliofungwa, kuna watu wanaoshindwa kuendelea, kuna watu wamekwama kwasababu ya magonjwa ya kurogwa na magonjwa ya kawaida, 

Isaya 33:28 inasema “Wala hakuna mwenyeji wa mtoto wa Mungu wa mbinguni atakayesema mimi ni mgonjwa au anaumwa. Mungu atasambaratisha katika jina la Yesu, kwani Yesu alichukua magonjwa yote msalabani na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 


Lakini kuna watu wabaya wanatuwinda sisi watoto wa Mungu, na sisi leo tunaenda kuwashughulikia. Tumezoea kusema, “Mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie la kulia”, mimi ninakupa pole. Mungu anasema, “Kisasi ni changu, niachie.” Wewe unamuambiaje Mungu wakati wa kumlipiza mtu kisasi. Unatakiwa kumwambia Mungu atazame unavyoonewa na maadui zako walikusababishia ukakwama na unashindwa kuendelea mbele, watoto walala njaa (aibu), watoto hawana school fees (aibu)

MAADUI WASIO NA SABABU KATIKA MAISHAN YAKO..
Tunatakiwa kutambua kuwa hata mimba ina maadui, barabara ina maadui,. Barabara ikiwa imenyooka utashangaa watu wanasema wekeni matuta. Je, Wewe ni nani usikose maadui. Kuna watu wanakutakia mabaya, kula ukifanya jema wanataka liharibike, ukivaa vizuri wanasaga memno, ukipendeza wanachukia, ukijenga nyumba nzuri wanakasirika, ukila nyama unajenga vita kati yao.

Kuna watu wabaya wameapa ya kuwa lazima wakuharibie, wakuvurugie mipango yako. Haya mambo yapo mitaani kwetu, na kama yapo tunafanya nini? Kuna watu wengi wako “against” na wachungaji wenzao, wanafanya jitihada kumharibia mchungaji mwezao,.

Unatakiwa kutambua Mungu yupo na lolote utakalo liomba Mungu atakupa. Pia ili kumshinda adui yako unatakiwa kuyajua maadiko ya Mungu.

Kuna walokole wenginwameapa ili waweze kukusamabaratisha ili maombo yako yasiende, wanakutupia magonjwa, wengine ni wakristo wenye imani ndogo ambao wanaenda hata kwa waganga pale wanapoona mabo yao hayaendi sawa.

JE, UNA SHIDA AMBAYO IMEKUG’ANG’ANIA?
Je, una tatizo la kudumu? Una ugonjwa ambao hutaki ukuachie? Je, Umekwama kwa namna moja au nyingine kwasababu ya mtu tu kakukwamisha? Je, unajitahidi kufanya kazi lakini umekwamishwa na wabaya wako?

Kuna watu wanakwamisha wenzao wasiendelee mbele, kuna watu wa,ewafungwa wenzao wasifanikiwe, kuna watu wanashindwa kuendelea kutokana na kuwekiwa kiuzibe na wabaya wao, kuna watu wamekwama kwasababu ya magonjwa ya kurogwa na magonjwa ya kawaida, umaskini, uvivu, kukosa kufikiria mbali, kujiona hawawezi, kutofanya kazi, kutomshirikisha Mungu kwa kila hatua, kutopenda kumtumikia Mungu. Watu hawa wamejikuta wakiyafanya hayo yote bila ya wao kujua. Maadui zao wamewafungwa wasiwaze maendeleo bali wazidi kuka tamaa na kuona hakuna kufanikiwa. 

Isaya 33:28 inasema “Wala hakuna mwenyeji wa mtoto wa Mungu wa mbinguni atakayesema mimi ni mgonjwa au anaumwa. Mungu atasambaratisha kila magonjwa, kila roho chafu, kila nguvu za giza, kila roho za kukata tamaa katika jina la Yesu. Mungu atayafanya haya yote kama tutamkubali na kumtumikia kutoka ndani ya mioyo yetu. Biblia ianatuambia "Yesu alichukua magonjwa yote msalabani na kwa kupigwa kwake sisi tumepona." Kwahiyo kama Yesu alichukua mateso yetu iweje wewe ubaki unateseka na kuhangaishwa na dunia hii? Yawezekana kuna mahali haupo vizuri na Mungu, shetani ana anatumia mwanya huo kukutesa kwa njia moja au nyingine 



Unatakiwa kutambua ya kuwa kuna watu wabaya wanatuwinda sisi watoto wa Mungu, na sisi leo tunaenda kuwashughulikia. Tumezoea kusema, “Mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie la kulia”, mimi ninakupa pole. Mungu anasema, “Kisasi ni changu, niachie.” Wewe unamuambiaje Mungu wakati wa kumlipiza mtu kisasi? Unatakiwa kumwambia Mungu atazame unavyoonewa na maadui zako walikusababishia ukakwama na unashindwa kuendelea mbele.

Yaani ni abui sana kuona mtu mzima mwenye nguvu na akili lakini watoto wake wanalala njaa, watoto hawana school fees, pesa hakuna, mtu hajajenga, mtu anadaiwa kodi ya nyumba, kula kwao ni mlo mmoja, magonjwa yameweka makao makuu mwilini mwake na mambo mengine mabaya kama hayo. Njia moja ya kuondoa hayo ni kujitathimini ni wapi hauko sawa na Mungu, na ukishapaona, amaua kuziba "gap" hilo mara moja.



na sisi leo tunaenda kuwashughulikia. Tumezoea kusema, “Mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie la kulia”, mimi ninakupa pole. Mungu anasema, “Kisasi ni changu, niachie.” Wewe unamuambiaje Mungu wakati wa kumlipiza mtu kisasi? Unatakiwa kumwambia Mungu atazame unavyoonewa na maadui zako walikusababishia ukakwama na unashindwa kuendelea mbele.

Yaani ni abui sana kuona mtu mzima mwenye nguvu na akili lakini watoto wake wanalala njaa, watoto hawana school fees, pesa hakuna, mtu hajajenga, mtu anadaiwa kodi ya nyumba, kula kwao ni mlo mmoja, magonjwa yameweka makao makuu mwilini mwake na mambo mengine mabaya kama hayo. Njia moja ya kuondoa hayo ni kujitathimini ni wapi hauko sawa na Mungu, na ukishapaona, amaua kuziba "gap" hilo mara moja.

-------------
Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare.
Ibada ya KUZAA MUUJIZA WAKO Iliyofanyika
Mlima wa Moto Mikocheni "B"


Siku ya Jumapili 02.09.2018


















































































Comments