26.08.2018: WATUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAKIABUDU KATIKA IBADA YA KUPIGANIWA NA BWANA

Enock Tontoo na Praise & worship Team ya Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walivyoweza kuwaongoza waumini wa kanisa hilo katika kipindi cha kumwabudu Mungu kilichofanyika siku ya Jumapili 26.08.2018 katika ibada ya KUPIGANIWA NA BWANA. Tulishuhudia uwepo wa Mungu, nguvu za Mungu wakati tukimuimbia Mungu wetu nyimbo za kuabudu. Hakika Mungu wetu hukaa katikati ya sifa.

Kupitia nyimbo hizi BWANA hufungua milango ya baraka kwa wale wamuimbiao kwa kumaanisha na wakiamini kile wanachokiimba. Nikuombe wewe ambaye ulikosa ibada ya Jumapili iliyopita, usikose kuhudhuria ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.


Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3
Enock Tontoo


















Comments