12.08.2018: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOHUBIRI KATIKA IBADA YA MAOMBI YA KUFUNGULIWA KATIKA VIFUNGO VILIVYOTUFUNGA TUSIFIKIE MALENGO YETU
MAMBO YAKUFANYA NA YATAKAYOKUTOKEA KWA MWEZI WA NANE NA MWEZI WA TISA 2018
BWANA apewe sifa. Leo nataka nikupe mambo muhimu ya kufanya katika mwezi huu wa nane 2018 na mambo yatakayotokea kwa mwezi wa tisa 2018. Kwanza naomba usikose ibada ya MAOMBI HATARI YA KUVUNJA LAANA NA ROHO ZINZOFUATILIA MAISHA YAKO siku Jumapili hii 19.08.2018 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Siku hiyo kutakuwa na maombi ya DERIVERANCE yaani maombi ya KUFUNGULIWA. Ni Jumapili ya kuwafungua watu kutoka katika vifungo vya mateso mbalimbali na umaskini. Na mwezi huu wa nane 2018.
Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare

































Pili napenda kukujuza kuwa kila Jumapili ya mwezi wa nane 2018 itakuwa ni Jumapili maalum ya kuwaombea watu mbalimbali ili wafunguliwe kutoka kwenye vifungo na kuwekwa huru, ni Jumapili ya maombezi tu. Kila Jumapili tutakuwa na tamasha la maombezi ambapo kila mtu atapeleka maombi yake binafsi kwa Mungu. Watumishi wa Mungu na mimi Bishop wake tutakuombea ili utoke katika shimo la mateso unayopitia kwa muda mrefu.
Kama unakumbuka tulisema, mwezi saba 2018 utakuwa ni mwezi wa KISULISULI., mwezi wa kuleta baraka kama vile gari lako, nyumba yako, mke wako, mume wako, kazi yako,, mafanikio yako, mitaji wako n.k. Tunamshukuru Mungu kwani watu wengi BWANA aliweza kuwabariki na maisha yao yanakwenda kama walivyopanga.

Kwahiyo mwezi wa nane 2018 ni mwezi wa kuondoa kila kipingamizi, kila laana, kila kamba iliyokufunga usisonge mbele, kila mnyororo uliokufunga. Mwezi huu tunaenda kuukata huo mnyoororo katika maisha yako ili upate mpenyo. Tunatamani Mungu afanye njia pasipo na njia katika maisha yako.
Mwezi wa tisa 2018 utakuwa ni mwezi wetu wa KUPOKEA MIUJIZA. Nataka kusikia kila nyumba, ofisi kuna vigeregere na shangwe zinazosababishwa na mafanikio waliyopata baada ya maombezi ya mwezi wa nane 2018. Kwahiyo mwezi wa tisa utakuwa ni mwezi wa kupokea majibu kutoka kwa BWANA. Lakini mwezi wa nane ni mwezi wa kupambana na kila kipingamizi katika maisha yako.

Mwisho, napenda kukualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.
UKIKOSA PESA, UNAKOSA UHURU
Naomba tusome Isaya 42:22-23 na Isaya 49:24. Unajua mtu ukikosa pesa unakosa uhuru kwasababu huwezi kununua kitu unachotaka, huwezi kwenda unakotaka, huwezi kula unachotaka, unaiona nyama buchani unaimezea mate tu, unasikia miji mizuri huwezi kusafiri. Kuna baba mmoja nilimuona akipita kwenye kiduka cha kuchoma kuku, akaona kuku wamebanikwa, wanazunguka kwenye mashine ya kukaushia, kuku wananukia na wanavutia. Baba yule akasimama kuwaangalia wale kuku kwa kutamani, na alipomaliza kuwaangalia akajifanya amezarau zile kuku kwasababu alikuwa hana pesa ya kununua wale kuku ilia wale. Baba Yule alikuwa amebanwa kifedha. Kama mtumishi wa Mungu niliumia sana. Mwezi huu BWANA anakwenda kukufungua katika utumwa wa kukosa pesa kwa jina la Yesu. Unachotakiwa kukifanya ni kumtumikia kwa moyo wako wote na kutenda yaliyo mema. Soma Neno la Mungu na lifanyie kazi ili likuongoze kufikia malengo yako na kuwekwa huru katika vifungo vya umaskini.

MAOMBI YA HATARI YA KUWAFUNGUA WATOTO WA MUNGU WALIOFUNGWA KATIKA VIFUNGO ILI WASIFANIKIWE
Tunasema Jumapili hii ya tarehe 12.08.2018 ni Jumapili ya kuwafungua wale wote waliofungwa kiuchumi na kroho. Kuna watu wapo mahali wamefungwa na wanashindwa kujitoa, watu wametekwa, watu wana misukosuko, watu wanamajaribu na hakuna mtu asemaye, “Waachie hao watu waliofungwa.”
Leo Mungu amenitume kama mtumishi wake nishuke katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” nimwambie na kumkemea shetani aliyefunga watoto wa Mungu ya kwamba, “Wewe shetani uliowafunga watoto wa Mungu popote ulipo achilia watu wa Mungu, warudishe watu wa Mungu kwani wao sio mateka bali hawa ni watoto wa Mungu wanahitaji kuishi maisha ya uhuru na amani. Naongea na wewe shetani ya kuwa ukate minyororo yako, kata kamba zako ulizozifunga kwa watoto wa Mungu kwa Jina la Yesu Kristo. Nakuteketeza kwa jina la Yesu. Ninaharibu mipango yako kwa jina la Yesu Kristo.

Je, Unafikiri watoto wa Mungu wameacha pombe bure, wameacha kuwa malaya na kusema “Take me good” kama machangudoa wanavyofanya mitaani bure? Je, Unafikiri hawana pesa ya kwenda kujirusha kweye ma-“club”? Nataka nikwambie wewe shetani kuwa hawa ni wateule, ni watoto wa Mungu, hawa wanapendwa na Mungu , wamejinya vyote ili waingie mbinguni. Kwa mamlaka niliyopewa na Mungu nasema, “Waachilie watoto wa Mungu kwa jina la Yesu, usiwaguse hawa kwani ni masihi wa Mungu”
USIKUBALI KUDANDIA MAGARI YA WATU USIOWAJUA…ANGALIA KILICHOMKUTA HUYU DADA KINASIKITISHA SANA.
Ukipata muda soma Isaya 42:22-23 na Isaya 49:24-25. BWANA anasema, “Watoto wangu wamekuwa mateka.” Kuna siku moja nilisikia ushuhuda wa dada mmoja ambaye alichukuliwa kwenye gari zuri baada ya kuomba “lift”. Wale watu waliompa "lift" kuna sehemu wakampeleka na alipofika eneo hilo wale waliompa “lift” wakasema, “Hapa sasa umefika, na hapa ni mahali ambapo watu wanafanyiwa unyama, wanafanyiwa mambo mabaya na wewe umejileta mwenyewe.” Yule dada alishangaa sana kusikia habari mbaya kutoka kwa hao waliompa "lift", akajiona yuko tayari kwenda kutolewa sadaka. Yule dada akaanza kuhangaika kutafuta “lock” ya kufungulia mlango wa gari ili aruke kwenye gari. Yule dada anasema, akabahatika kufungua ule mlango wa gari na akaruka kwenye gari na kudondoka kama gunia, akaamuka na akakimbia mbio. Dada yule akaanza kushuhudia kwa watu ya kuwa alikuwa ametekwa bila ya yeye kujua, alidhani yule mwanaume aliyempa "lift" na baadae kumteka alikuwa ni mtu mwema kumbe sio. Anasema, "Nilidhania amenipa “lift” tu kumbe anataka kuniua, na huyo mwanaume alikuwa na maneno matamu wakati naongea naye kabla hajanipeleka eneo la tukio."

Nachotaka kukumambia ni kwamba, “Kuanzia sasa Koma sana kutamani magari ya watu na kuomba “lift”, koma kabisa kuona “handsome boy” wanaendesha gari na wewe ukadandia na kujipendekeza kwake. Dunia ya sasa watu wamebadilika, sio kila mtu ni mwema wengine ni wabaya.
Na katika maisha ya sasa kuna watu wametekwa bila ya wao kujijua. Kuna watu wamewateka kwa kwenda kwa waganga ili wawaloge. Kama mtumishi wa Mungu ninasema, “Leo lazima utoke kwenye uteka katika jina la Yesu Kristo. Kuna watu wametekwa bila kujijua na wakajikuta wamejiingiza kwenye uzinzi, umalaya, wizi, uongo, usengenyaji, ulevi, uasherati na sehemu mbalimbali. Kuna watu wametupia maroho ya giza na kujikuta mtu anaanza kubadilika na kuwa na tabia isiyompendeza Mungu. kama mtumishi wa Mungu ninasema kwa jina la Yesu ninakutoa huko kwa damu ya Yesu. Kama unaamini sema, “Amina”

KUNA WATU WAMEANZISHA MAKANISA NA KUWA AJIRI WATU ILI KUIBA WAUMINI WA MAKANISA MENGINE.
Kuna watu wameanzisha makanisa na kuwa ajili watu ili wawachukue waumini wa kanisa fulani na kwenda katika makanisa yao. Inashangaza kuona kuna watu wengi sana katika kanisa letu la Mlima wa Moto Mikocheni “B” na ndani yake kuna watu wameajiliwa na makanisa mengine kuja kuwaiba waumini wetu na kuwapeleka katika makanisa yao.
Watu hawa walioajiliwa na makanisa mengine kuiba waumini wanapewa pesa na kuambiwa “Kama utaleta kichwa kimoja kanisani nitakupa Tshs. 50,000/=. Kwahiyo wanafanya kila njia kuwaiba waumini ili mradi wamepata pesa.

Watu hawa bila huruma hawajui mimi nimehangaika kiasi gani kuhakikisha waumini wangu wanakuwa kanisani. Bila aibu na woga anakuja kuwalaghai waumini wangu kwa pesa zake. Hawajui ya kuwa kitu wanachofanya sio mapenzi ya Mungu.
Siku zingine huwa nalala na viatu kitandani nikiwaombea waumini wangu ili wazidi kuja kanisani kujifunza Neno la Mungu lakini watu wasio na huruma wanatuma watu kuja kanisani kwangu na kuwadanganya waumini wahame kanisani. Kuna baadhi ya waumini wengine ni wachanga kiroho, wakiona hivyo wanaamini na kuwafuta hao wezi wa waumini. Wengine kutokana na shida ya pesa nyumbani kwao wanaamua kukubali ili mradi wamepata pesa.

Kama mtumishi wa Mungu ninasema, “Hao wanaotuma watu na wanaotumwa, BWANA akawafilisi, wakafilisike na wasifanikiwe kwa lolote kwa jina la Yesu Kristo. Kwasababu wanachofanya ni kuharibu huduma ya mtu mwingine. Lakini kama Mungu alinipa watu, basi ataendelea kunipa wengine mpaka watashangaa.
Kuna njia nyingi za kupata waumini na sio kuiba waumini wa watu wengine ambao wamenolewa na watumishi wake kwaajili ya kuujenga mwili wa Kristo wakiwa katika huduma waliyokulia. Kama unahitaji waumini kwanini usiandae mikutano Jangwani au mahali popote ili watu waokoke na waje kanisani kwako kwa hiari kuliko kutuma watu kuja katika kanisa la mtu mwingine na kuwalaghai waumini kwa pesa zako. Wapo watu wengi sana mitaani wanatamani kuja kanisani lakini wanakosa watu wa kuwatia moyo na kuwafundisha utamu wa Yesu katika maisha yao.

Kuna watu wako nje ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” wanatamani sana kuabudu nasi lakini kuna watu wengine wabaya wapo humu ndani ya kanisa letu wametumwa na watumishi wengine kkwaajili ya kuwahamisha waumini wetu kwa pesa zao na wengine wanatumia vinywa vyao kwa kusema maneno mabaya kuhusu kanisa ili watu wakate tamaa ya kuabudu katika kanisa letu. Utasikia watu wabaya wanasema, “Unajua siku hizi hata muumini fulani amehama hili kanisa kwasabau sio kanisa sahini.”
Nataka kukuuliza, “Itakufaidia nini au itakusaidia nini kama watu wakiondoka kanisani na ukabaki peke yako? Je, unaweza kusali peke yako baada ya watu kuhama katika kanisa letu? “Are you happy” unapoona mtu kahama kanisa kwetu? Je, Huumii unapoona mtu kahama kanisa kwako?. Kila mahali umekuwa ni mtu wa kuharibu kanisa kwa umbeaumbea wako. Kila mtu akikuona anakukimbia na kukutenga kwa tabia yako mbaya ya kuhamisha watu na maneno yako ya uchonganishi.

Ninasema kama mtumishi wa Mungu niliyepewa mamlaka na Mungu yakuwa, “Ukorofi lazima uondoke kwa jina la Yesu, tunang’oa roho ya ukorofi kwa jina la Yesu.” Mungu atuhurumie kama kanisa.
Lakini leo nina habari njema, ukisoma Isaya 49:24. Je, Aliyejabari anaweza kunyang’anywa mateka yake? Je, Watu waliofungwa wanaweza kuokoka kama hakuna mtu wa kuowafungua? Na mimi kama mtumishi wa Mungu ninasema, “Haijalishi umeteseka kwa miaka mingapi, adui yako amekufunga katika sehemu uliyonayo kwa miaka mingapi? Kwasabau Neno la BWANA linasema, BWANA atakuja na nguvu na atawapokonya mateka kwao waliohodari, atawanyang’aya mateka wote waliokuwa wamefungwa na uchawi, ndumba, manuizo, magonjwa, yatakuachilia kwa jina la Yesu.”

Ninaagiza moto wa Yesu Kristo kutoka mbinguni, ushuke kila mahali walipokufunga kamba, minyororo, kama ni pembeni ya bahari, kama ni kwenye mto; moto wa Mungu kateketeze kamba na minyororo kwa jina la Yesu.

TUKISHIKAMANA KAMA KANISA TUTAUJENGA MWILI WA KRISTO.
BWANA apewe sifa. Kama waumini na tunayetamani kwenda mbinguni tushikamane na tulijenge kanisa la Mungu, tusimamishe kanisa la Mungu, tuwajenge watu wanaokuja kanisani, tuwatie moyo, tuwape maneno mazuri ya Mungu, tuwapende watu wanaokuja kanisani na kuwakumbatia, tuwaongoze njia sahihi ya kwenda mbinguni, tuwafundishe jinsi ya kusimamia woko wao. Kila siku huwa natamani watu wanaokaa nyuma ya kanisa wangekuja kukaa mbele na sisi tulio mbele tukakaa nyuma ili nao waone utamu wa kukaa mbele karibu na madhabahu ya Mungu. Kuna watu wengine tangia wameanza kuabudu nasi hawajawahi kukaa mbele na wanatamani kukaa mbele. Na pia ningekuwa na uwezo ningetamani kuwakumbatia kila muumini katika kifua chake kama ishara ya upendo kwao. Kama kanisa tuonyeshe upendo kwa watu kama Kristo alivyotuagiza. Katika kanisa kusiwe na makundi ya watu kwani sisi sote ni watoto wa Mungu na safari yetu ya kwenda mbinguni ni moja tu. Unapoona mwingine hana nguo basi mpe nguo ili naye avae apendeze, unapoona mwezako analia na njaa nyumbani kwake basi mpe chakula, unapoona mwenzako hana nauli ya kuja kanisani au kwenda kanisa basi msaidie.

Kanisa letu la Mlima wa Moto Mikocheni “B” linajulikana kuwa ni kanisa la kimataifa, kanisa lenye upendo, kanisa lenye mshikamano, kanisa linalowajali watu wote, kanisa lililojaa uwepo wa Mungu. BWANA ametuvika utukufu kwahiyo tunapaswa kutunza hii "status." Muumini wa kanisa hili hata akifaa nguo yake ya kawaida anapendeza kwasababu anaye Yesu ndani yake anayempendezesha kwa kila jambo anapoonekana mbele za watu. Kwa kibali hiki alichotupa katika kanisa letu tunapaswa kumshukuru huyu Mungu wetu kwa kuwapenda wana Mlima wa Moto Mikocheni “B”.
Tuzidi kumtumikia Mungu, Kusona Neno lake, Kuliishi Neno lake, Kumsifu Mungu wetu, Kufanya maombi, kuwa na upendo kwa kila mtu, kuacha kutenda mabaya na kutenda mema, kujituma katika kazi ya Mungu, kulitangaza neno la Mungu, kuwasaidia wenye uhitaji, kutembeleana wakati wa shida na raha na mambo mengine kama hayo.
JIFUNZE KUPITIA NDOTO YA MTUMISHI WA MUNGU MAREHEMU TIRDO KUTOKA MAREKANI
Kuna mhubiri mmoja mkubwa sana kutoka Marekani anaitwa marehemu Tirdo. Siku moja aliota ndoto ambapo aliona shetani amevaa nguo ya kikahaba, amejipamba kikahaba akaona anaingi katika nyumba ya mtu wa Mungu. Watoto waliokuwa katika ile nyumba wakaanza kumfukuza na kumkea wakisema, “Toka kwa jina la Yesu, Toka Roho ya uzinzi kwa Jina la Yesu.” Yule dada ikabidi atoke haraka. Mtumishi wa Mungu akaota ndoto tena na akaotoa roho ya madhaifu; akaona mtu akitembea kwa mwenda wa udhaifu huku akiingia kwenye nyumba ya mcha Mungu, na aliofika hapo wale wacha Mungu wakaanza kukemea wakisema, “Toka roho ya magonjwa, roho ya madhaifu hauna mamlaka kwa jina la Yesu. Baada ya kumaliza kukemea ile roho ikakimbilia mbali. Akaota tena roho ya umaskini, akaona mtu amevaa suruali yenye kilaka, miguu imejaa vumbi tupu, anakuja amechoka mbaya, na alipofika kwa wacha Mungu akaomba wamfungulie aingie ndani. Wacha Mungu baada ya kuona Yule maskini wakamfungulia aingie ndani kwasabu alikuwa ni maskini na wao wanajua maskini na tajiri wataingia mbinguni. Je, Katika ndoto hii unajifunza nini?

Hivi ndivyo ilivyo katika makanisa ya sasa, kama watumishi wa Mungu tunatakiwa kuwaombea wagonjwa na kuwawekea mikono wagonjwa wetu, kila mtu anatakiwa kuwa “concern” kuomba wagonjwa na makahaba ili nao waingie katika ufalme wa Mungu.
Inasikitisha kuona wacha Mungu siku hizi wameacha kuomba kwaajili ya kuondoa umaskini, wapo "busy" na maombi ya kukomesha magonjwa tu wakati umaskini unawatesa wengi. Ni vyema kuombea afya zetu na kumuomba Mungu atuepushe na magonjwa lakini pia tusishau kuomba kwaajili ya kukomesha umaskini. Unapokuwa huna pesa ni rahisi sana kuwa na mawazo hasi katika maisha yako ambayo yatakupelekea kutenda dhambi ili upate pesa.

Unatakiwa kutambua kuwa roho ya umaskini, roho ya uhitaji, roho ya kuombaomba sio sehemu yako wewe uliyeokoka na unayemtumikia Mungu kwa uaminifu. Kuna watu wanakuja kanisani kwaajili ya kuwaomba watu wengine pesa kwa kuwadanganya kuwa hawana hata nauli ya kurudia nyumbani. Ukiona mtu katika kanisa letu la Mlima wa Moto Mikocheni “B” akiomba nauli, mfukuze kwasababu kanisa linatoa nauli kwa waumini wote wasio na nauli ya kurudia majumbani kwao baada ya ibada. Mungu akubariki sana.
TUNAKEMEA LAANA NA MAGONJWA YA KURITHI KUTOKA KWA MABABU
Fikiria usemi huu, “Kuna baadhi ya wababa wamekula ndimu lakini meno ya watoto yamekufa ganzi.” Tukiwa wadogo tulikuwa tukila maembe mabichi na meno yetu yalikuwa yakifa ganzi. Pia mtu akila ndimu nyingi memno yake yanakufa ganzi. Maana ya usemi huu ni kwamba, kuna magonjwa ya kurithi ambayo ni laana ya ukoo. Ukiwa na mimba ukienda kwa daktari anakuuliza, “Katika ukoo wenu mna magonjwa gani?’” Unapotaja magonjwa yako kwa daktari naye anayaandika ili baadae kama kuna ugonjwa utakutokea, basi itakuwa rahisi kujua kama ugonjwa huo ni wa kurithi.

Inasikitisha kuona kitoto kidogo kinazaliwa na kinabanwa na pumu aliyoambukizwa kwa baba yake kabla ya hata kuvuta hewa chafu. Kuna magonjwa ambayo watu wanarithi kutoka kwa mababu kama vile “pressure”, kufa kabla ya wakati, ulevi wa kukithiri, kutokuolewa, kuachika katika ndoa, kupewa taraka, na mengine kama hayo. Lakini kama wewe umeamua kuokoka kwa dhati na kumtumikia Mungu kwa bidii, kile kitovu cha laana na magonjwa ya kurithi kinakatika na ungana na kitovu cha Yesu, unaungana na watu wa mbinguni, unakuwa katika familia ya watoto wa Mungu, magonjwa ya kurithi hayatakuja kwako na yakija kwako lazima uyakatae
IMANI YAKO NDIO ITASABABISHA KUYASHIDA MAPITO YAKO.
"Hakuna gumu kwa Mungu, yote yanawezekana kwake aaminie." Ukiamini mateso yote yanaondoka na ndio maana sisi tuliokoka tunampenda Mungu kwasababu tumemuamini na Yeye anatutkelezea yale tunayoyaomba kwa wakatiaujuaye Yeye. Inasikitisha kuona mtu aliyeokoka ambaye ameacha anasa zote za dunia halafu anakuja kuumwa magonjwa ya kurithi kama vile kisukari , "pressure" n.k. Na ukiona hivyo basi ujue kuna mahali mtu huyo hajaenda kama Mungu apendavyo. Na baadhi ya watu wanaumwa kisukali na ukiwauliza utasiki wakisema, “Unajua hiki kisukari ni changu”. Watu kama hawa hanwana imani na Mungu kuhusu uponyaji, wamekata tamaa, hawamtegemei Mungu, imani yao ni hafifu kuhusu uponyaji, maombi yao haya nguvu ya kumgusa Mungu kushusha uponyaji katika afya zao. Mara nyingi nikisikia hivyo huwa najisikia vibaya. Inauma sana kuona wenzako wanarithi mali, wameachiwa majumba na wazazi wao lakini wewe unarithi kisukari, pressure na magonjwa mbalimbali ya kurithi. Kama mtu uliyookoka lazima ukatae hali ya kurithi magonjwa ya ajabu ajabu kwa jina la Yesu kwani sisi ni watoto wa Mungu tuliyeokoka na tunatakiwa kurithi mali na sio magonjwa. Mungu anasema, “Enyi maadui msiwaguse hawa masihi wangu ni watu wa kuogopwa sana.” Sisi ni kama wanyama wale wakubwa duniani yaani The Big Five (Simba, Twiga, Zebra, Tembo n.k). kwahiyo hatutakiwi kushambuliwa na wachawi ambao wanatutumia roho za magonjwa katika afya zetu. Kama watoto wa Mungu tuliyeokoka hutupaswi kuguswa na mabaya, tunatakiwa kuwa na afya njema. Mchawi anapotaka kuloga watu waliokoka mara nyingi hupata shida sana kwasababu wana ulinzi wa Mungu, wanamesimama na Mungu, wanamuamini Mungu, wanaongozwa na Roho Mtakatifu.

Wakati naishi Mikocheni, kuna baba mmoja kila asubuhi alikuwa akiniita, “mama wa Kipogolo”, nikimwitikia, ananiuliza, “Kuna mtu yeyote amelazwa hapa?” Nilikuwa nadhani huyu baba ni mwanga au mchawi. Kumbe huyu baba usiku analoga watu na asubuhi akiamuka anategemea kusikia kuna mtu amelazwa hospitalini. Siku zingine ananiita, “mama wa Kipogolo, Je, umetokea moto eneo hili? Kumbe usiku aliona moto wa Roho Mtakatifu ukiwa umezunguka nyumba yangu kwahiyo wachawi wakija hawanioni bali wanaona moto umenizunguka.
Kwahiyo ukitaka kuyashinda majaribu unapaswa kumtumikia huyu Mungu, kumuamini, kumtii, kuachana na mabaya, kutenda yaliyo mema, kuwasaidia wenye uhitaji, kuwa na upendo kwa kila mtu, kushiri ibada ili kujifunza Neno la Mungu na mambo mengine mema kama hayo.
Comments
Post a Comment