11.07.2018: MCH. MAINA KUTOKA KENYA AONGOZA MAOMBI KATIKA SEMINA YA SIKU 8 YA MID YEAR CROSS OVER -MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mtumishi wa Mungu Mch. Baraka Maina kutoka Kenya alivyosamabaratisha kazi za shetani katika semina ya siku 8 za Mid Year Cross Over 2018 inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kila siku kuanzia saa 9:30 alasiri.

Maombi haya yalifanyika siku ya Jumatano 11.07.2018 ikiwa ni siku ya 4 tangia semina hii ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka kuanza. Watu wengi sana waliona nguvu za Mungu na wengi wao kufunguliwa kupitia mtumishi wake Mch. Mainah. Baadhi ya watu walifungwa na nguvu za giza, kuota ndoto mbaya, kuonewa, kufukuzwa kazi, kutoapata kazi, kutozaa, kutopata mimba, kuharibikiwa mimba, matengano katika ndoa, magonjwa sugu, masengenyo, kutopenda Neno la Mungu, kukataliwa na mengine kama hayo, lakini baada ya maombi haya BWANA alianza kufungua milango polepole kwa baadhi ya watu. Na wale ambao bado kufunguliwa tunategemea kabla ya mwaka kuisha tutasikia shuhuda mbalimbali za watu wakimshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoyafanya kupitia semina hii ya Mid Year Cross Over 2018.

Mungu amekuwa mwema sana kupitia semina hii. Tumeshuhudia Mungu akiongea nasi kupitia watumishi wake na kutupa mawazo mapya ya kumjua Mungu na zaidi ya yote tunapata mawazo mapya kwaajili ya maisha yetu ya kila siku. BWANA anazidi kitufungulia milango ya mafanikio katika maisha yetu kwasababu tunamtumikia na kutii maagizo yake kupitia watumishi wake.

Wewe ambaye hujabahatika kushiriki semina hii iliyozinduliwa na Mtumishi wa Mungu Bishop Dunstan maboya kutoka Arusha siku ya Jumapili 08.07.2018, unayo nafasi nyingine ya kufika hekaluni mwa BWANA ili ukutane na mkono wa Mungu utakaokuvusha hapo ulipo na kufikia malengo yako ya mwaka 2018.

Hii ni semina ya kumshukuru Mungu kwa mwezi sita iliyopita na kukabidhi miezi sita iliyobaki kumaliza mwaka 2018 mbele za Mungu. Kuna vitu vingi vibaya na vyema vilivyo mbele yetu na sisi kama wanadamu ni ngumu kuvijua lakini kwasababu tunaye Mungu naye atatuonyesha na kutukamilishia sawasawa na haja ya mioyo yetu. Ni wajibu wetu wa kuzidi kumtumikia huyu Mungu bila kuchoka tukiwa bado tuna pumzi. Tuzidi kuomba Roho Mtakatifu akae ndani yetu ili atuongoze katika njia sahihi dhidi ya maadui zetu. Tunapaswa kujitakasa mioyo yetu ili Roho wa Bwana akae ndani yetu kwani Roho wa BWANA hawezi kukaa mahali pachafu. Tutajitakasa kwa kutenda mambo mema na kuwa karibu sana na Mungu wetu aliye hai.


Naomba siku ya leo usikose semina hii saa 9:30 alasiri na siku ya Jumapili 15.07.2018 itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na itakuwa ndio hitimisho la semina hii mpaka mwakani (2019)

Mch. Baraka Maina kutoka Kenya

















Comments