08.07.2018: MAMBO YATAKAYOTOKEA BAADA YA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2018 INAYOENDELEA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCH ENI “B”

BWANA YESU APEWE SIFA !Tunaingia katika wiki la kongamano la Kumshukuru Mungu kwa miezi sita iliyopita na kukabidhi miezi sita iliyobaki kumaliza mwaka 2018 mbele za BWANA. Unaposikia miezi sita ni kama msitu, huwezi kujua ni nini kitatokea kwa miezi sita iliyo mbele yako, kwahiyo ni vizuri kuanza kwa unyenyekevu na BWANA. Katika miezi iliyo mbele yako kama hauko vizuri na Mungu utakutana na mikosi mingi sana na kama uko vizuri na Mungu utakutana na Baraka nyingi kutoka kwa Mungu mwenyewe. 

Soma Hesabu 11: 30-32 Ninajua kabisa kwa miezi sita iliyopita ulikuwa ukifunga, ukiomba kwaajili mahitaji yako ya kimwili na vile vile mahitaji ya kiroho. Kuna kitu ulikuwa unakihitaji lakini kimekawia kufika. Kuna wakati umekata tama kutokana na ndoto zako kutotimia kwa wakati unaotaka. Nataka nikuhakikishie ya kuwa leo Jumapili 08.09.2018 tunaanza kongamano la Mid Year Cross Over 2018 ni lazima BWANA atafanya jambo la kushangaza katika maisha yako baada ya siku saba za semina hii ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka.

Wana wa Israel walikuwa na kanisa jangwani na walikuwa na uhitaji lakini walikuwa wanakula mana yaani mikate kutoka mbinguni. Baada ya kula mikate kwa muda mrefu ile mikate ikawakinai wakata kula chakula kingine kama vile,nyama. Wakamwambia Musa tunahamu ya nyama, naye Musa baada ya kuambiwa hivyo akanung’unika sana. Mungu akamwambia Musa, “Je, mkono wangu ni mfupi? Mbona mimi ninaweza.” Musa alipoingia kambini, upepo wa kisulisuli ulitoka magharibu, mashariki, kaskazini na kusini na ule upepo wa kisulisuli ulileta kwale (kuku wa porini) ambao ni watamu kuliko kuku tunaowafuga majumbani. Mungu alivuta kwale kwaajili ya wana wa Israel nao wana wa Israel wakawaokota na kula nyama yao mpaka wakashiba.

Na ndivyo ninavyokutabilia ya kuwa kwa siku hizi saba za semina hii, kama mtumishi wa Mungu, ninaenda kuvuta mujiza wako, ninaenda kukuletea unachokihitaji, ninaenda kukomesha uhitaji wako wa pesa, uhitaji wako wa mtaji n.k. Mungu atatenda jambo na utafurahi. Mungu atakukumbuka kwa jina l Yesu. 

Wana wa Israel walidhani wamesahauliwa, lakini Mungu alisikia kilio chao. Na leo Mungu anakwenda kusikia kilio chako, kile kilicho mbali BWANA atakivuta, wale wadeni wako wasiopenda kukulipa kwa upepo wa kisulisuli wataleta pesa yako waliyokopa. Mungu hatakuacha kama ulivyo. Ninaona muujiza wako kwa jina la Yesu, ninaona Baraka zikishuka kwa jina la Yesu.

Na mimi ninakuambia, “Hudhuria kwa uaminifu hizi siku saba mpaka Jumapili 15.07.2018 utaona mkono wa BWANA katika maisha yako.” Kama Mungu hatatenda jambo katika maisha yako, njoo unishike gauni na uniulize. Baada ya miezi mitatu tarajia miujiza kwa maana, “Anything caha happen any time.” Wewe kaa mkao wa kula chakula cha BWANA baada ya semina hii ambayo inaendlea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kuanzia saa 9:30 alasiri na siku ya Jumapili itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Walete wenye uhitaji na Mungu mwenyewe kupitia watumishi wake atashughulika na maisha yako.
------------
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Mlima wa Moto Mikocheni "B"





Mahubiri ya Jumapili 08.07.2018

 Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare

















































































Comments