08.07.2018: BISHOP DUNSTAN MABOYA AKIZINDUA RASMI SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER

Baada ya kusubiri kwa hamu semina hii ya MID YEAR CROSS OVER 2018, hatimaye siku ya Jumapili 08.07.2018 Bishop Dunstan Maboya akishirikiana na Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare tuliweza kuzindua rasmi kwa maombi na baadae tukaweza kukata utepe.

Semina hii hufanyika mara moja tu kwa mwaka kwa lengo la Kumshukuru Mungu kwa kutulinda kwa miezi sita tangia mwaka uanze na kumkabidhi Mungu miezi sita iliyobaki kumaliza mwaka.

Hii ni semina ambayo watu wengi hufika kwaajili ya kumkumbusha Mungu kwa yale amabayo bado hayajatimia katika maisha yao na kumshukuru Mungu kwa kuyatimiza baadhi ya malengo waliyoyapanga kwa mwaka mzima na pia kwaepusha na mabaya yote yaliyotokea kwa kipindi cha miezi sita.

Kwa muda wa siku saba, tumekuwa katika kufunga na kuomba kwaajili ya semina hii na juu ya maisha yetu, kwahiyo watu watakaokanyaga katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kushiriki semina hii ya siku 8 ambayo imeanza Jumapili tarehe 08 na kuhitimishwa Jumapili 15.07.2018 watakuwa wa tofauti sana kuanzia kimwili na kiroho. Watapokea nguvu za ajabu sana, imani zao zitakuwa, hofu ya kumpenda Mungu itaongezea, watapata mafanikio ya mwili n.k.

Tumeona watu wengi walioshiriki semina hizi kwa miaka iliyopita wakipata kazi, wakioa na kuolewa, wakipata watoto, wakipata mimba, wakijenga, wakinunua magari, wakipandishwa mishahara, wakifungua miradi mikubwa, wakipata tenda, wakifaulu masomo yao, wakipata safari za Ulaya zenye mafanikio, wakiponywa, wakiunganishwa na watu waliofanikiwa, wakibuni miradi yenye mafanikio, wakilindwa na ajali mbaya, huduma zao zikiongezeka, wakijazwa nguvu mpya na Mungu, wakifarijiwa wakati wa changamoto, wakipata matumani katika mateso yao, wakifunguliwa katika nguvu za giza na mambo mengine kama hayo.

Unachotakiwa kukifanya ni kuchukua hatua za kufika hapa kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B", huku ukiamini kutedewa na Mungu na kuyashika yale utakayoambiwa na watumishi wa Mungu na kuyatendea kazi. BWANA hatakuacha kutokana na juhudi zako za kumtafuta. Jinsi unavyojituma kumtafuta Mungu na kufanya yale anayotaka ndipo naye Mungu anapozidi kukufungulia milango yako ya mafanikio.

Tenda yaliyo mema na utaona mkono wa BWANA katika semina hii. Semina inaanza saa 9:30 alasiri kwa siku za katikati ya wiki na siku ya Jumapili itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Walete wenye shida mbalimba na BWANA atawasaidia kwa Jina la Yesu Kristo.

Katika wokovu wangu sijawahi kuona mtu anayemtafuta Mungu kwa bidii akiishi maisha ya taabu. Mimi ni ushuhuda tosha, kwani tangia nimemjua huyu Mungu na kuanza kumtumikia sijajuta katika maisha yangu. Kila kukicha ananipeleka viwango vingine. Natamani na wewe baada ya semina hii, BWANa akukufikishi angalau nusu yangu au zaidi yangu kimafanikio. BWANa asikuche katika mateso ya umaskini bali akuinue katika viwango vya juu.

Tuonane baadae mwanangu. Mungu akusaidi upate nauli ya kuja kanisani, akupe mafuta katika gari lako, akupe ruhusa kwa boss wako, akupe moyo wa kumpenda Mungu, akupe wepesi wa kuja kanisani siku ya leo saa 9:30 alasiri.

Bishop Dunstan Maboya akikata utepe
























Comments