08.07.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKA NA KUBATIZWA KWA MAJI MENGI SIKU YA KWANZA YA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2018

Ikiwa ni siku ya kwanza kati ya siku nane za Semina ya Mid Year Cross Over 2018, ambapo siku ya Jumapili 08.07.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" watu wengi sana waliweza kuokoka na kubatizwa kwa maji mengi. Mch. Asenga akishirikiana na wainjilisti waliweza kuwabatiza na kuwaombea waongofu wapya. Baada ya kubatizwa na kujazwa na Roho Mtakatifu, siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao za kuanza mafundisho ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri.



Tunakuomba sana uzidi kuwaombewa ili wakivamiwe tena na huyu ibilizi mwovu. Ombea afya yao, kazi zao, familia zao na maisha yao mapya ya wokovu.

Kumbuka semina hii Kumshukuru Mungu kwa miezi sita iliyopita na kukabidhi nusu mwaka kwa Mungu itahitimishwa siku ya Jumapili 15.07.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". siku za katikakti ya wiki itakuwa ikianza saa 9:30 alasiri na siku ya Jumapili itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Wanenaji na Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Mch. Sylvanus Komba na Apostle Francis Musili kutoka Kenya.

TUONE KWA UFUPI UBATIZO WA MAJ MENGI NINI?

01.Ubatizo wa maji mengi ni nini au ni upi?
Ubatizo wa maji mengi unamaanisha ya “zamisha ndani ya maji mengi” . Ni kitendo cha imani ch kushiriki kifo cha Bwana Yesu kwa kuzamisha ndani ya maji na kufufuka pamoja naye kwa kupandishwa kutoka kwenye maji mengi.

Warumi 6:4-5. “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.” Wakolosai 2:12. Kumbuka ; Ubatizo ulifanywa kwa maji mengi- Yoh.3:23

a) Ubatizo wa Yohana mbatizaji.
Yohana mbatizaji yeye alibatiza kwa maji mengi (Yoh.3:23) Na ubatizo wake ulilenda juu ya:

Toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi (Matendo 13:24,Luka 3;3). Kuwaandaa watu kumpokea Yesu (Luka 7;29-30,Yoh.1;23)
Kutangaza wazi juu ya wokovu pamoja na ghadhabu kali ya Mungu ( Mathayo 3;12)
Ubatizo wa Yohana mbatizaji ulitofautiana na ubatizo wa Ki-kristo. Kwa sababu ubatizo wa Yohana mbatizaji ulikuwa ni ubatizo wa toba huku ubatizo wa kikristo umelenga kwanza kumuamini na kumpokea Bwana Yesu awe Bwana na mwokozi kwa abatizwaye na abatizwe katika Yeye Bwana Yesu. ( Matendo 19:4-5). Ni muhimu sana kujua hilo.

2. Faida za Ubatizo wa Maji mengi:-
- Kutimiza sehemu ya agizo kuu la Bwana -(Mathayo 28;18-19)
- Kuzifia dhambi -( Warumi 6 :4)
- Kusababisha chimbuko la dhamiri safi mbele za Mungu (1 Petro 3:20-21)
- Kumvaa Kristo ( Wagalatia 3:27)
- Kupata nguvu mpaya za rohoni katika utumishi wako ( Mfano ni kwa Yesu,ambaye hakuanza huduma mpaka alipobatizwa )
- Kuchochea karama yako
- Kuponya kwa magonjwa (Ninazo shuhuda hapa,ukinipigia nitakueleza kiurefu) n.k
- Roho mtakatifu,Yesu na Mungu baba hushuka kushuhudia ubatizo huo na kumwaga nguvu ( Mathayo 3:13-17 nafsi zote tatu zilihusika)

3. Ubatizo wa maji mengi unafanyika vipi?
- Katika maji mengi – Yoh.3:23
- Katika Jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu- Ingawa mitume walibatiza kwa Jina la Bwana Yesu ( Matendo 2:38,19:5) Lakini leo tunabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu.
- Ni ibada kamili kama ibada nyingine yenye kiongozi,na lazima iheshimiwe. n.k
Majina,ardhi ya kwenye maji ni lazima itakaswe kwa damu ya Yesu kabla ya kuanza ubatizo. - -
- Pia ikiwepo kuna majina mapya ya kutumika kwa wabatizwa,ni lazima yaombewe kikamilifu.
Wabatizwa wazamishwe Rohoni kabla ya kubatizwa,na kuomba ni lazima ili kumruhusu Roho mtakatifu afanye kazi yake.
n.k

Nikushukuru kwa kupata ndondoo chache za Ubatizo wa maji mengi. Usipange kukosa semina hii. Usafiri wa kufika kanisani siku za katikati ya wiki ni bure kuanzia Mwenge kwenye mtaa na siku ya Jumapili usaifi utakuwa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3


Mch. Asenga









































































Comments