01.07.2018: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOHUBIRI KATIKA IBADA YA MAOMBI YA HATARI YA KUBOMOA NGOME ZINAZOZUIA KUFIKIA MALENGO YETU NA KUKOMESHA LAANA

BWANA Yesu apewe sifa. Leo sina mambo mengi ya kuongea na wewe kuhusu ibada ya Jumapili ya tarehe 01.07.2018 bali nimeona ni vyema nikakuandalia video ya mahubiri ya Ibada iliyofanyika Jumapili iliyopita ya "Maombi ya Hatari y Kubomoa Ngome Zilizozuia Kufikia Malengo Yako na Kukomesha Laana Zote zilizotamkwa Juu Yako." Ibada hii ilifanyika siku ya Jumapili 01.07.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kuhubiriwa na mimi mtumishi wako Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Tunamshukuru Mungu kwa mwitikio mkubwa sana wa watu waliofika kuabudu nasi, na hii inatokana na matunda wanayopokea katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ukiona watu wanakimbilia mahali unatakiwa kujua kuna kitu kinawavutia na kinawanufaisha katika maisha yao na afya zao. BWANA amekuwa mwaminifu sana katika huduma hii kupitia watumishi wake aliowachagua kwa kazi yao. Wengi waliombewa na kuwekewa mikono na wakaamini, BWANA ahakuawaacha bali aliwashika mkono na kuhakikisha anatimiza ahadi zake kwa wakati wake.

Kwahiyo, ninaamini ukiangalia hizi video mbili, tegemea kupokea muujiza wako kama utayachukua yale utakayoyasikia na kuyafanyiakazi katika maisha yako. watu wengi wanasikia sana mahubiri na wanaombewa sana lakini hawapokei miujiza yao, moja ya sababu ya kutopokea miujiza yao ni kwamba kile wanachofundishwa hawakifanyii kazi, hawakiishi, hawakitendei haki, wepesi wa kusahau, hawakithamini, hawaamini, mioyo yao ni migumu, wamezoea mahubiri n.k. Lakini wale walioamini na kuyafanyia kazi mahubiri ya watumishi wa Mungu, wengi wao wamefanikiwa na sasa wanafurahia wokovu na maisha yao ni ya amani na furaha.

sasa, nimekuandalia video mbili.
1. Video ya kwanza bonyeza hapa: 

2. Video ya pili bonyeza hapa

Wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada hii na ungetamani kufanyiwa maombi na kujifunza Neno la Mungu ili likusaidie kumjua Mungu na ukishamjua Mungu uapate kupokea baraka zake. Karibu Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Siku ya Jumapili usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3

Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare


















































Mch. Stanley Nnko










































Comments