24.06.2018: WACHUNGAJI WAFANYIWA MAOMBI NA KANISA ZIMA KATIKA IBADA YA KURUDISHIWA UTAKATIFU ULIOIBIWA NA KUVISHA VAZI LA UTUKUFU

Katika ibada ya KURUDISHIWA UTAKATIFU ULIOIBIWA NA KUVISHWA VAZI LA UTUKUFU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa 
Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 17.06.2018, waumini na watumishi mbalimbali wa kanisa hili waliweza kuwaombea wachungaji wote wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kuwatamkia baraka katika huduma yao, famili zao na kazi zao. 

Kama Wakristo tunawajibu mkubwa sana wa kutenga muda kwaajili ya kuwaombea watumishi wa Mungu., kwani wao ni mabalozi wa Mungu walioletwa duniani kwaajili ya kutangaza Injili ya Mungu na kuhakikisha roho za watu zinaokolewa. Kwahiyo ni vema ukatenga muda kwaajili ya kuwaombea ili wazidi kutuhudumia katika maisha yetu.

Mungu anawatumia watumishi hawa kutuletea habari njema kutoka KWAKE, kutuombea, kututamkia baraka, kutulea kimwili na kiroho, kutushauri tunapomkosea Mungu, kutufariji tunapopitia magumu, kutuongoza katika njia sahihi ya kwenda mbinguni, kutosogeza karibu na Mungu, kutukumbusha kutenda yaliyo mema, kutuongoza sala za toba, kutubatiza, kubariki ndoa zetu, kufungisha ndoa zetu, kuliombea tafa amani na utulivu, kuwaombea viongozi mbalimbali n.k, kwahiyo wanahitaji sana maombi yako. pale unapopata nafasi au pale unapokuwa katika maombi yako usisahau kuwaombea watumishi wa Mungu. 

Mwisho napenda kukualika katika ibada ya Jumapili katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3asubuhi hadi saa 8 mchana.


Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3








































Comments