24.06.2018: MAMA WACHUNGAJI WA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAFANYIWA MAOMBI KATIKA IBADA YA KURUDISHIWA UTUKUFU


Siku ya Jumapili 24.06.2018 katika ibada ya KURUDISHIWA UTAKATIFU ULIOIBIWA NA KUVISHWA VAZI LA UTUKUFU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kulikuwa na maombi maalum kwaajili ya kuwaombea wake za wachungaji (mama wachungaji) wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kanisa zima liliweza kuwaombea na kuwatamkia baraka pamoja na familia zao. Tunamshukuru sana Mungu kwa kutoa maono haya ya kuwaombea watumishi wa Mungu ambao wamefanyika mchango mkubwa sana kwa wachungaji.

Wewe ambaye ulikosa ibada hii tunakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3






Comments