20.05.2018: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS KWAYA ZAFANYIKA BARAKA KATIKA IBADA YA KUIOMBEA FAMILIA

Siku ya Jumapili 20.05.2018 katika ibada ya KUIOMBEA FAMILIA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ikiongozwa na Bishop Mhe. Gertrude Rwakatare, kulikuwa na kwaya ya Happy Kwaya na Joybringers ambazi zilifanyika baraka sana kwa nyimbo zao zenye kufundisha, kuadibisha, kuelimisha na kufariji. Hakika kupitia nyimbo zao tuliona uwepo wa Mungu katika ibada hiyo. Tuzidi kuziombea Kwaya hizi ili zizidi kumtumikia Mungu na kutuhudumia kiroho kupitia karama zao za uimbaji. Kupitia sauti zao tunafarijika, tunaondoa usongo wa mawazo, tunaburudika, tunainuliwa kiroho, tunabarikiwa na kuwa na hofu ya Mungu. Nyimbo zao zinatufanya kuwa karibu sana Mungu kwasababu Mungu wetu ni Mungu anayependa sana kuona watu wake wakimsifu na kumuimbia nyimbo zenye kumtukuza. 

Kwahiyo huduma walionayo ina mchango mkubwa sana katika maisha yetu na familia zetu. Tunapaswa kuyasikia yale wanayotuimbia na kuyafanyia kazi katika maisha yetu. Kumbuka hawa ni watumishi wa Mungu na mabalozi wakubwa sana wa Mungu ambapo wanatuwakilishia ujumbe wa Mungu kupitia nyimbo zao.

Wewe uliyekosa ibada hii, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. 

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3

Happy Kwaya



Joybringers Kwaya

























Comments