20.05.2018: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOHUBIRI JUU YA FAMILIA ZETU

JITAMBUE WEWE NI KUHANI
Tunatakiwa kujitambua kuwa sisi tuliyeokoka ni watumishi wa Mungu na ni makuhani wa Agano Jipya, kwahiyo tunatakiwa kila siku tujitakase ili tunaposimama mbele za BWANA tuweze kuwa na nguvu ya kuambukiza Utakatifu kwa watu wengine bila kujali dini, kabila, taifa la mtu, wewe unachotakiwa ni kuambukiza ucha Mungu na sio kumuambukiza maovu katika maisha yake. Jina lako linatakiwa kuwa kama la Joshua (soma Zakari 3:3, utaona Joshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, lakini alikuwa akisimama mbele ya malaika, mbele ya kanisa, mbele madhabahu, na mbele za watu wacha Mungu kwaajili ya kazi ya BWANA. Usijidharau, BWANA ameweka kitu ndani yako kwaajili ya kuokoa maisha ya watu. Kama Kuhani unatakiwa kujipanga, kujiamini na kuhakikisha unalijua Neno la Mungu kwaajili ya kuokoa maisha ya watu.
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare


KATAA KUVAA VAZI LA AIBU
Ukisoma Zakaria 3:3 Joshua alikuwa amevaa vazi chafu sana, kwahiyo na wewe unatakiwa kujiangalia umevaa vazi gani? Kuna wengine wamevalishwa mavazi machafu sana na maadui zao au na mababu zao. Kuna wengine wamevalishwa vazi la magonjwa, madeni, kukataliwa, , kuota ndoto mabaya, nguvu za giza, kutozaa, mimba kuharibika, kushindwa masomo, madeni, kuonewa kwa kila analofanya, kunyoshewa kidole vibaya mpaka anahisi kunyeshewa mvua n.k. Watu kama hawa wamevishwa vazi baya na wanahitaji msaada wa Mungu kupitia watumishi wa Wake ili kuondoa aibu na kuvunjiwa heshima katika jamii. Kuna watu wameabishwa mbele za watu, mbele za watoto, mbele za marafiki zake kutupiwa nguvu za giza na zikasababisha magonjwa sugu, ukichaa, umaskini, kufedheshwa, kutengwa na mambo mengi mabaya. Lakini nataka nikuambie kuwa yupo Mungu anayejua shida zako. Wewe mtazame Yeye huku ukiwaamini watumishi wake utaona mkono wa huruma ukivua vazi lako chafu na kukuvisha vazi safi lililobeba miujiza yako.



JIVUE VAZI LA UMASKINI
Kwa kipindi kirefu umekuwa ukiteswa na maadui zako ambao walikuvisha vazi chafu kama alilolivaa Joshua kama tunavyosoma katika Biblia (Zakaria 3:3). Kupitia vazi hilo umejikuta kila unalofanya halifanikiwi. Kazi unayofanya hailingani na kipato unachopata, malengo yako hayatimii na kama yanatimia sio kwa wakati uliotaka yatimie, maendeleo yako ni ya kusuasua. Kama mtumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, kwa msaada wa Mungu leo ninakuvua vazi la umaskini na kukuvisha vazi la kuinuliwa kiuchumi na hautachekwa tena eti kwasababu hauna pesa, hautadharauliwa tena kwa jina la Yesu, madeni yote yatayeyuka kwa jina la Yesu. Kama unaamini sema, “Amen” Watu wamekuvika vazi chafu la hasira (kila wakati unakasirika), vazi chafu la kudharau wengine na kujiona wewe ni bora kuliko watu wengine, umekuwa mtu wa kutoa kasoro kwa wengine na kujiona wewe ni mtakatifu wakati ni muovu kama wengine. Unafanya vitu vibaya bila kujitambua bali unajihesabia haki. Leo hii ninaondoa hali ya kutotambua mabaya yako na kujihesabia haki. Amua kubadilika sasa, ili upone. 



EPUKA KUHUKUMU WENGINE
Kuna watu wengi wamevishwa mavazi machafu na maadui zao, wamekuwa ni watu wkuhukumu wengine kama vile wao ni Mungu. Mwenye juhukumu la kuhukumu wanadamu ni Mungu tu. Kabla hujahukumu angalia kibanzi kwenye jicho lako ndipo utoe uhukumu yako batili, Mungu wetu anahukumu kwasababu Yeye ni msafi hana doa la uovu, bali sisi wanadamu tuna madoa ya maovu, kwahiyo hatupaswi kuhukumu watu wengine bali kuwafundisha njia sahihi ya kwenda mbinguni kwa Baba. Kabla yakumnyooshea kidole mwezako unatakiwa kutambua kuwa kuna vidole vinne vitakunyooshea wewe. Kwahiyo uwe makini sana na yale unayotamka kwa mtu mwingine yasije yakakurudia mwenyewe. Unavyomtendea mabaya mwenzako leo hii, ujue kesho yatakukuta makubwa zaidi hayo. Ukiona umetendewa baya basi piga maogti na peleka mashitaka yako kwa Mungu. Mungu wetu ni Mungu wa haki na ni hakimu wa kweli, atakupa majibu yako na kutoa hukumu ya kweli kati yako na aliyekukosea.



USIKUBALI LAANA ZA MABABU ZAKO ZIKUANGAMIZE
Katika laana za mababu kuna matatizo yanayotokana na ukoo. Kuna baadhi watu vijijini wakitaka kuoa/kuolewa wanauliza ukoo gani wenye tabia nzuri kuoa/kuolewa. Na kuna baadhi ya watu vijijini wananuiza na kutamka maneno mabaya katika familia za watu wengine ili ziisiwe na mafanikio au mabinti zao wasiolewe. Na ndio maana utakuta familia moja imejaa na talaka, mambinti wameachika au wengine wana laana za ulevi, ugomvi, kutozaa, magonjwa sugu ya kurithi, mambinti warembo wana miguu kama chupa lakini hawaolewi, vijana wazuri lakini hawaoi, vijukuu vimelundamana kwa mababu zao kutokana na kuelekezwa na wazazi wao, watoto wadogo kuugua pumu, matatizo mengine kama hayo, Ukiokoka lazima ujiondoe na huo msululu wa laana za mababu kwasababu usipojiondoa huo mlolongo unakufuata hata kwenye kizazi chako. Unatakiwa kusimama mwenyewe na kukata hizo kamba za laana za kurithi katika familia yako. Sio kila mtu anatamani kukuona umefanikiwa, wengine wanakesha kwa waganga na kukunenea maneno mabaya. Nakusihi Rudi kwa Yesu sasa, Amua Kumtumikia...

WIVU UTAKUPONZA
Katika maisha tunayoishi kuna watu wapo kwaajili ya kuvunja mioyo ya watu wengine. Kila kukicha wao ni kukatisha tamaa wengine ili wasisonge mbele kiroho na kimwili. Wanapokuona umenunua gari, umejenga nyumba, umeoa au kuolewa, umepandishwa cheo au mshahara, umepata kibali, una amani katika familia yako, mambo yako yanakunyookea, unamtumikia Mungu kwa uaminifu; basi wao wanakasirika na kufanya jitihda za kukushusha ili uwe maskini na umtumikie shetani. Watu kama hawa wamekosa hofu ya Mungu, shetani amewatawala. Wewe uliyevunjwa moyo na kukatishwa tamaa; Nataka nikuambie ya kuwa hakuna mtu mwenye mbingu ila Mungu tu, na aliyekuita ni Yesu tu ambaye alimwaga damu yake kwaajili yako ili uwe huru na siku ya mwisho ukakutane na Mungu, kwahiyo jipe moyo na songa mbele. Usijaribu kuharibu ndoto yako kwaajili ya mtu tu. Na wewe unyeumwa na uko kanisani, nakutia moyo kuwa wewe changamka kwani Yesu alichukua magonjwa na yupo kukusaidia. Biblia inasema, Kwa kupigwa kwake Yesu wewe ni mzima. Bwana anasema, “Tafuteni nanyi mtapa”


kwahiyo katika hayo magumu unayopitia mtafute Mungu kwani yeye anapatikana na yuko tayari kukusaidia. Na wewe unayemnyima raha mwezako, chamoto utakipata

...................
Bishop Hon. Dr. Gertrude Rwakatare.
Mlima wa Moto Mikocheni “B”Assemblies of God
Member of ICCEBA - USA.
May 20.2018





















































































Comments