06.05.2018: MAOMBI KWA WENYE UHITAJI WA WATOTO YAFANYIKA KATIKA IBADA YA MAOMBI YA ONGEZEKO MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

06.05.2018: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": WANAOHITAJI WATOTO

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walivyopata nafasi ya kuwaombea watu waliokuwa na uhitaji wa kupata watoto. Kwa muda mrefu wamehangaika kupata watoto lakini imeshindikana. Kuna wengine walikufuru na kwenda hata kwa waganga ili wapate watoto lakini ikawa ni ngumu kupata kile walichokuwa wakihitaji. Baada ya mateso hayo wakaamua kuja nyumani mwa BWANA na kukutana na mabalozi wa Mungu hapa duniani, nao waliweza kutii agizao la Mungu la kuwaombea watu wenye mahitaji yao ili watimize ndoto zao.

Maombi haya yalifanyika siku ya Jumapili 06.05.2018 katika ibada ya maombi ya ONGEZEKO yaliyofanyika katika kanisa la Ishara na Miujiza la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Yawezekana unapitia changamoto kama hizi, na umehangaika sana bila majibu. Nikualike katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" ufanyiwe maombi na wapakwa mafuta wa Mungu. Kuna watu wengi walikuja wanalia kulingana na shida zao lakini BWANA aliwafuta machozi na sasa wanafurahia UKUU wa Mungu. Pengine Jumapili hii ni zamu yako ya kufutwa machozi. nakuomba uje kanisani ukiwa na imani ya kupokea muujiza wako. Waamini watumishi wa Mungu, amini Neno la Mungu, watii watumishi wa Mungu, soma Neno na ish katika Neno, acha maovu bali tenda yaliyo mema. BWANA anakupenda kwahiyo onyesha upendo kwa Mungu ili aweze kuwa karibu na wewe wakati wa shida na raha. Acha kumzoea Mungu, au kuzoe ibada bali fanya kama ni kitu kigeni kwako. Mungu anakupenda na wewe enndelea kumpenda Mungu na watu wake bila kuchangua dini zao, makabila yao, imani zao, mataifa yao, rangi zao. Tukutane kanisani Jumapili hii.
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare





































Comments