29.10.2017: MCHUNGAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" NA MKE WAKE WAKIMSHURU MUNGU KWA KUWAVUSHA KATIKA JARIBU NDANI YA FAMILI

Baada ya kupitia changamoto katika familia yao, wamshukuru Mungu kwa kuwatia nguvu. Hii ilifanyika siku ya Jumapili 29.10.2017 katika ibada ya maombi ya KUTENGUA MANUIZO NA LAANA KATIKA MAISHA YA WATU ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Mungu wetu ni MUngu wa huruma na upendo. Unapopitia magumu Yeye anakutia nguvu na kukupa muongozo mwingine kutimiza malengo yako na kusahahu yale yote uliyoyapitia.

Yawezekana unapitia changamoto fulani katika maisha yao na imefika kipindi unajiona ni mtu wa kuchanganyikiwa, unatamani kujiua, hutamani kusikia Neno la Mungu, umekata tamaa, umekosa amani, umekuwa ni mtu wa kujitenga na kujidharau, mahudhurio ya kushiriki ibada yamepungua na mengine kama hayo, Ndugu yangu nataka nikutie moyo kuwa yupo Mungu anayeweza yote. Jitahidi kufika katika ibada zetu za Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.











Comments