29.10.2017: WALIOKOKA KATIKA IBADA YA KUTENGUA MANUIZO LA LAANA KATIKA MAISHA YA WATU ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hawa ni baadhi ya watu au waongofu wapya walioamua kwa hiari zao kuokoka na kupokea Yesu Kristo kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yao siku ya Jumapili 29.10.2017 katika ibada ya maombi ya Kutengua Manuizo na laana katika maisha ya watu. Tukio hili lilitokea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Mch. Elizabeth Lucas aliwaongoza sala ya toba na baadae wachungaji wa kanisa hili waliwaombeana kupelekwa mahali maalum kwaajili ya kubatizwa kwa maji mengi.


Kipindi wakiombewa, kuna baadhi yao waliangushwa chini huku mapepo na majini yakipiga kelele yakitaka kuondoka kwasababu yalikutana na moto wa Mungu. Na hii ilisababishwa na nguvu za Mungu na uwepo wa Mungu uliotanda katika kanisa hili.

Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku yao ya kujifunza masomo mbalimbali ya kukulia wokovu ambayo hutolewa bure katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Baada ya kumaliza masomo yao, waongofu hawa hufuatiliwa na wachungaji na wainjilisti wa kanisa hili kwa kuwatia moyo na kusikiliza matatizo yao katika safari ya wokovu.

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" linahitaji sana watu wengi kuja kuokoka na kubatizwa siku za Jumapili ambapo ibada huanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kwahiyo unayo nafasi ya kumpokea Yesu kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako.


Wewe ambaye umeokoka unao wajibu wa kuwatafuta watu mtaani kwako ambao hawajaokoka na kuwashawishi wafike kanisani ili waokoke na wafurahie maisha mema ya wokovu kama unayoyafurahi. Unajua unapookako unakuwa na uhakika wa kufika kwa Mungu kama utakuwa unaishi maisha mema kama wokovu unavyotaka.

Kutakuwa na usafiri bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada kumalizika utarudishwa kituoni.
Mch Elizabeth Lucas



































































Comments