29.10.2017: WAIMBAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAMSHUKURU MUNGU KWA MAJARIBU WALIYOPITIA KATIKA FAMILIA YAO

Waimbaji hawa ambao ni wanandoa (mume ni mwimbaji wa kwaya ya Happy Kwaya na mke wake ni mwimbaji wa Praise & Worship Team) wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walimshukuru Mungu kwa yale yote waliyopitia katika familia yao. Mungu aliweza kuwavusha na kuwatia moyo pale walipooumia mioyo yao. Walimshukuru sana Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maombi yake ambayo yalifanyika baraka katika kipindi kigumu walichokuwa wakipitia. Kupitia maombi hayo waliweza kupata faraja na kutiwa nguvu ya kusonga mbele.

Pia walimshukuru Mungu kwa watoto aliowapa ambao wamefanyika baraka katika maisha yao. Hii ilifanyika katika ibada ya maombi ya Kutengua Manuizo na Laana katika Miasha yetu iliyofanyika siku ya Jumapili 29.10.2017 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"







Comments