29.10.2017: JINSI WATU WALIVYOMTUKUZA MUNGU KWA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa siku ya Jumapili 29.10.2017, tulimuona Mungu akishughulika nasi katika kipindi cha kusifu na kuabudu. Tulibarikiwa na uimbaji kutoka kwa Mch. Prisca Charles pamoja na Praise and Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Ibada hii ilikuwa ni ibada ya Kutengua Manuizo na Laana katika maisha yetu ambayo iliongozwa na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare pamoja na jopo la wachungaji wa kanisa hili. Watu walijifunza mambo mengi juu ya kutengua manuizo na laana na pia walipata muda wa kuombewa.


Tunakushukuru wewe uliyeshiriki ibada hii na tunatumaini yale yote waliokunuiza na kukutamkia laana yote yameondoka na sasa uko huru kumuabudu Mungu wako wa mbinguni. Tunahitaji kusikia shuhuda kutoka kwako.

Pia tunawakaribisha watu wote katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana itakayofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".
Mch. Prisca Charles





Mzee Mwakitalu


















ANGALIA VIDEO

Comments