22.10.2017: MWANAKWAYA YA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" AMSHUKURU MUNGU KWA UPONYAJI

Kaka huyu alimshukuru sana Mungu kwa uponyaji mkuu alioufanya Mungu katika maisha yake. Kabla hajapata tatizo la kutotembea alikuwa ni mwanakwaya wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa muda mrefu lakini baada ya kupata tatizo hili alishindwa kuendelea kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji kutokana na ugonjwa aliokuwa nao. Kaka huyu ameteseka sana maumivu makali katika kiuno chake na magongo kwa muda mrefu, lakini hakukata tamaa, alizidi kumuamini Mungu na kuweza kufika kanisani kwa kubebwa. Siku ya Jumapili 22.10.2017 katika ibada ya KUHARIBU NGUVU ZA KAFALA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" alimshukuru Mungu kwa uponyaji mkuu. Hivi sasa anaweza kutembea mwenyewe na anajiandaa kuendelea na masomo yake Dodoma.

Yawezekana na wewe umekuwa kitandani kwa muda mrefu, umekuwa mtu wa kubebwa, kulishwa, kuogeshwa na umehangaika kwa waganga, kwa madaktari na hospitali mbalimbali lakini hujapata uponyaji wowote. Umekuwa ni mtu wa kilia na pengine kumkufulu Mungu wako, ndugu na marafiki yako wamekuacha, hawataki hata kukusaidia kwa lolote lile lakini nina habari njema ya kuwa YUPO Yesu Kristo atakayetatua shida yako. Hakuna analoshindwa Mungu wetu wa mbinguni kwani yeye ndiye aliyetuumba na anajua system ya miili yetu. Wewe ni kukaa na Mungu na kumg'ang'ania mpaka uone mwisho wake, usikate tamaa wala usikatishwe tamaa na wanadamu.

Muombe Mungu akupe nguvu za kuweka kufika hapa kanisani au muombe mtu wa akulete katika hekalu la Mungu la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili uombewe na mtumishi wake Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la watumishi wa Mungu waliopo hapa kanisani. Wapo watu wengi sana walikuja na magonjwa mbalimbali lakini walipokanyaga madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" magonjwa yao yaliyeyuka na sasa ni wazima wa afya wanafurahia wema wa Mungu.

Pia unatakiwa kuwa na ile IMANI kuwa Yesu Kristo anaponya magonjwa, unatakiwa kutubu dhambi zako, kuacha kutenda maovu, kumtegemea Mungu, kusoma Neno la Mungu, kufanya maombi na kufunga, kuwapenda watu wote, kuacha chuki, kumtolea Mungu, kushiriki ibada za kila siku kanisani na kutenda yale yote anayotuagiza katika amri zake 10. Mungu ni mwaminifu kama na wewe utakuwa mwaminifu kwake. Muangalie Mungu na kumtegemea katika jaribu lako unalopitia kwa sasa, naye atakuvusha salama.

Ibada Jumapili hii itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Ninakuombea Jumapili hii tukutane katika nyumba ya Mungu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili tuombe kwa pamoja.














Comments