22.10.2017: MWANAFUNZI AMMSHUKURU MUNGU KUMALIZA MASOMO YAKE YA SHUKE YA MSINGI

Siku ya Jumapili 22.10.2017 katika ibada ya maombi ya KUHARIBU NGUVU ZA KAFALA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Dada huyu alimshukuru Mungu kwa kumfanikisha katika mitihani yake ya mwisho ya kidato cha sita na sasa anategemea kujiunga na chuo. Dada huyu alishindwa kupata maneno ya kuzungumza ikabidi aanze kuimba tu kumshukuru Mungu kwa matendo makuu katika masomo yake.

Mungu wa mbinguni kupitia huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" amekuwa akiwabariki na kuwainua wananfunzi katika masomo yao na mitihani yao. Wapo wengi sana wanafanikiwa masomo yao baada ya kuombewa na watumishi wa Mungu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", na baadae kupata kazi nzuri.

Pengine umekuwa ukishindwa kufanya vizuri  masomo yako na mitihani yako kwa muda mrefu. Umehangaika kwa waganga, makanisa mbalimbali na hujaona mpenyo wowote, ninaomba nikukaribishe katika madhabahu ya miujiza ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukutane na nguvu za Mungu kutoka kwa Mungu kupitia mtumishi wake "Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopola wachungaji, wainjilisti na walimu wa kanisa hili. Usihangaike, wewe njoo ukiwa na ile IMANI ya kupokea majibu chanya kutoka kwa Mungu.

Ibada ya Jumapili hii itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usipange kukosa. Usafiri ni bure kutoka kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kweye mataa barabara ya Coca Cola na baada ya ibada utarudishwa kituoni.











Comments