22.10.2017: MAELFU YA WATU WANYA DAMU YA YESU KATIKA IBADA YA KUAHARIBU NGUVU ZA KAFARA ZILIZOFANYIKA NA WABAYA WETU KATIKA MAISHA YETU

Hivi ndivyo mapepo, majini, roho chafu, nguvu za giza zilivyokuwa zinateseka baada kukumbana na moto wa Yesu ulao ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 22.10.2017. Siku hii ilikuwa ni siku maalum kwaajili ya maombi ya KUHARIBU NGUVU ZA KAFARA ZILIZOFANYIKA KATIKA MAISHA YETU (UFUNUO 12:11).

kabla ya maombi kuanza Mch. Noah Lukumay aliweza kufundisha juu ta DAMU YA YESU. Sasa tuone baadhi ya point alizozifundisha siku hiyo, alisema:-

-Damu ya Yesu huondoa kafara, inabeba uzima, huondoa wachawi, inatupa ujasiri wa kwenda mbele na Mungu, huondoa hukumu, ni ya thamani na hakuna mtu ambaye anaweza kulipa gharama yake, inatupa upatanisho kati yetu na Mungu - Waebrania 12:24, inatunenea mema, inaondoa mapepo na majini na nguvu za giza, inafanya kazi kuliko akili za mwanadamu, inaoondoa maadui wenye lengo la kukuharibia, inaondoa vita, inaondoa hofu na mashaka, inaondoa magonjwa, inatupa ushindi, inaondoa nuksi na mikosi na mambo yote mabaya. 

- Unatakiwa kuuitia damu ya Yesu kwa kila jambo unalolifanya, na kuna vitu inatakiwa tujitenge navyo ili maisha yetu yasonge mbele. Usikubali kutembea BILA damu ya Yesu Kristo ili kujikinga na maadui zako wanaotaka kukuahribia maisha yako. Ukiwa na damu ya yesu maadui zako wanabaki kuwa na hasira na wewe.

Baada ya neno fupi, Mch. Noah Lukumay pamoja na wachungaji wengine wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni walianza maombi ya kuharibu nguvu za kafala. Wakati maombi yakiendelea, baadhi ya watu walianza kutokwa na nguvu za giza, mapepo na majini kama unavyoona katika picha hapo chini.

Uwepo wa Mungu ulitawala kanisa zima na watu wakaanza kufunguliwa na nguvu za giza.

Yawezekana maisha yako ni ya mashaka, maisha yako yametawaliwa na nguvu za giza, mapepo na majini, umeandamwa na magonjwa sugu kwa miaka mingi. Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.






























































Comments