22.10.2017: KWAYA YA WOCA ILIVYOMTUKUZA MUNGU SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

//Mathayo 4:10: Msujudie BWANA Mungu wako, umwabudu Yeye peke yake.//

Katika ibada ya KUHARIBU NGUVU ZA KAFARA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 22.10.2017 maelfu ya watu waliungana na kwaya ya wazee (WOCA) ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakimsifu Mungu na kumwabudu Mungu kwa njia ya uimbaji. Kwaya hii imefanyika baraka katika kanisa na kwa watu wengi waliosikia nyimbo zao. Mungu ameweka mafuta ya upako katika nyimbo zao na ndio maana zimetokea kupendwa na maelfu ya watu. Watu wengi wametokea kuzipenda nyimbo hizi kutokana na ujumbe unaoimbwa na ile "Anointing" ambayo Mungu ameiweka kwa waimbaji hawa. Ukisikiliza nyimbo zao unabarikiwa na kama ulikuwa na usongo wa mawazo unafarijika. Kupitia nyimbo hizi watu wanainuinuliwa kiimani na zinaleta ule uwepo wa Mungu unapozisikiliza na kutafakari ule ujumbe wanaouimba. Siku ya Jumapili waliimba wimbo wao wa Kiganja cha Yesu na watu waliupokea wimbo huu kwa kishindo cha ajabu.


Waimbaji hawa wamejitoa kufanya kazi ya Mungu ndani ya nyumba ya Bwana ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili mimi na wewe tufike mbinguni. Kila unapowaona wakiimba wanaonekana wapya kwasababu Yesu anawafanya kuwa wapya ili sisi tuzidi kubarikiwa.


Kama utasukumwa na Mungu, tunaomba utenge muda wako kwa kuwaombea wanakwaya hawa katika huduma yao hii waliyoianza, iombee huduma yao, familia zao, kazi zao, afya zao ili wazidi kufanya kazi ya Mungu kwa moyo wote na kwa kujituma kama walivyoanza. Katika maombi yako usisahau kuwatamkia baraka katika huduma yao hii na katika maisha yao ya kila siku. Unapowaombea naye Mungu anakukumbuka katika maisha yako.


Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana watakuwepo kukubariki katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B", kwahiyo njoo mapema ili upokee upako kupitia kwaha hii.


Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni walikokuchukua.























Comments