20.10.2017: WAZAZI WA WANANFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAKIWAOMBEA WATOTO WAO KATIKA IBADA YA KUHARIBU NGUVU ZA KAFALA

Wazazi wa wanafunzi wa kidato cha nne siku ya Jumapili 22.10.2017 katika ibada ya KUHARIBU NGUVU ZA KAFALA ZILIZOFANYIKA KATIKA MAISHA YAETU, waliweza kufika katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwaajili ya kuwaombea watoto wao. Mch. Noah Lukumay, Mch. Elizabeth Lucas pamoja na jopo la wachungaji wa kanisa hili waliweza kuwaombea mafanikio katika  masomo yao na pia kuwaombea maisha yao yawe ya amani, pia waliwaombea wazazi ili waweze kupata unafuu wa kuwalea watoto wao. 

Tunamshukuru sana Mungu wetu wa mbinguni kwasababu amekuwa muaminifu kwa kila maombi ambayo watu wake wamekuwa wakiomba katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu wengi wamekuwa wakifika hapa kanisani wakiwa na vilio vyao mbalimbali, lakini Mungu wetu ni Mungu wa huruma kwa kupitia mtumishi wake Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na watumishi walio chini yake amekuwa akijibu maombi yao na kuwatimizia kulingana na haja ya mioyo yao.

Yawezekana ni una watoto unawasomesha, na wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali katika masomo yao. Pengine wamekuwa wakifeli masomo yao, hawaelewi kile wanachofundishwa, wamekata tamaa ya kuhudhuria masomo, wamefukuzwa shule kwa tabia mbaya, wamefukuzwa shule kwa kukosa ada kutoka kwa wazazi au walezi wao, wametupiwa mapepo na majini, wanateswa na nguvu za giza, wamelogwa, wamejiingiza katika ulevi na uvutaji wa madawa ya kulevya, wamenenewa mabaya na rafiki zako au majirani zako ili wasifaulu masomo yao, wanateswa na magonjwa na mambo mengine kama hayo. Nataka ni kwambie yupo Yesu Kristo mtenda miujiza katika huduma hii ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" atakaye wasaidia wanao. 

Jitahidi kufika hapa kanisani katika ibada zetu za Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana au katikati ya wiki kuanzia saa 9 alasiri utakutana na watumishi wa Mungu watakaowaombea wanao na ili  damu ya Yesu iwalinde katika masomo yao yote na maisha yao yote. Tunamshukuru sana Mungu kwani wapo wanafunzi wengi wamefunguliwa baada ya kufanyiwa maombi  katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".  Chukua hatua sasa za kufika katika kanisa hili ili maisha ya watoto wako yakawa ni maisha mepesi na wakafurahia masomo yao wakiwa na afya njema kimwili na kiroho.

Mungu wetu ni Mungu wa kusikiliza vilio vya watu, mahitaji yao na akishayasikiliza ni mwepesi wa kuyajibu kulingana na ombi la mtu kwa watu auonao Yeye. Kwahiyo unahitaji kumuomba Mungu bila kuchoka mpaka uone ombeni lako limetimia. Usiwe mtu wa kukata tamaa unapoona majibu yako hayajajibiwa kwa wakati uutakao wewe. Mungu wetu ni Mungu anajibu kwa wakati wake na kwa watu wake. Ili uwe mmojawapo wa watu wa Mungu, ni kutubu dhambi zako, kubatizwa, kusoma neno lake na kulifanyia kazi (kuliishi), kushiriki ibada mbalimbali, kujitoa kwa kazi za Mungu, kuwa mtoaji kanisani, kusaidia wenye uhitaji kwa chochote, kumpenda kila mtu bila kubagua dini, kabila, rangi au taifa lake na mambo mengine mema kama hayo.

Mungu akubariki sana.

Mch. Antony Mwakibete (koti la blue)














































Comments