01.10.2017: MCH. DKT. PETER MITIMINGI ATOA SABABU ZA KUTENGENEZA JINA NA UTAMBULISHO KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI (WOKA)


Mch. Dkt. Peter Mitimingi siku ya Jumapili 01.10.2017 ambayo ilikuwa ni siku ya hitimisho la Kongamano la Wanawake na Uchumi la Kukomesha Kilio Cha Mwanamke lililoandaliwa na Chama Cha Women For Christ Alliance (WOCA) aliweza kufundisha somo liligusa mioyo ya wengi, na leo tumeonna ni vyema tukakushirikisha ili na wewe upokee upako huo. Hivi ndivyo alivyofundisha.

VIZUIZI VITANO VILIVYO MKABILI MUSA NA KUTAKA KUMZUIA ASIPIGE HATUA KWENDA MBELE

KIZUIZI CHA KWANZA CHA MUSA:

MIMI NI NANI? – UTAMBULISHO – THE IDENTITY

(Kutoka 3:11)

“Musa akamwambia Mungu, mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israel watoke Misri?”

1. Musa alisumbuka juu ya UTAMBULISHO wake.

2. Hakujisikia kama alikuwa ANASTAHILI.

3. Alifikiri Mungu alichagua mtu asiye SAHIHI.

ZINGATIA MAMBO HAYA NI MUHIMU SANA KWAKO

1. Tengeneza utambulisho wa JINA lako vizuri.

2. Jina lako likikaa vizuri utaingia mahali wengine hawaingii.

3. Jina lako likikaa vizuri linaweza kukulisha wewe na vizazi vyako vya mbele.

4. Ndio maana makampuni mengi na taasisi nyingi zinztumia gharama kubwa kutengeneza jina lao maana wanajua ndani ya jina zuri kuna kila aina ya fulsa za mafanikio.
Mafanikio ya kwanza ya mtu yanaanzia kwenye kujitambua kwanza yeye ni nani – Self-image kisha yanakwenda kwenye utambulisho wa wengine wanamtambua yeye ni nani – Public Image.

KWANINI NI MUHIMU KUTENGENEZA JINA NA UTAMBULISHO WAKO?

1. Jina Zuri Ni Bora Kuliko "Perfume" ya Thamani.

Mhubiri 7:1 1 Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa. "A good name is better than fine perfume..."

2. Mungu Alimuahidi Abrahamu Kulikuza Jina Lake

Mwanzo12:2 Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

WATU WANATAKA KUJUA JINA LA MBEBA UJUMBE KABLA YA KUTAKA KUJUA UJUMBE ALIO UBEBA

1. Watu wanataka kujua jina la mwenye biashara au jina la kampuni kabla ya kujua bidhaa yenyewe.

Kutoka 3:13 - 14

13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu;(That was the message) nao wakaniuliza, JINA LAKE N'NANI? Niwaambie nini? 14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.

2. Fanya mambo yatakayo fanya jina lako (utambulisho wako ukae vizuri.

3. Kabla jina lako halijaanza kukulisha lazima wewe uwekeze kwenye kulilisha jina lako kwanza.

SOMO LILIENDELEA
















































































Comments