17.09.2017: MCH. NOAH LUKUMAY KATIKA IBADA YA MAOMBI YA KUFUFUA VITU VYETU VILIVYOKUFA ILIYOFANYIKA JUMAPILI

Siku ya Jumapili 17.09.2017 Mch. Noah Lukumay alifanyika baraka sana katika ibada ya MAOMBI YA KUFUFUA VITU VYETU VILIVYOKUFA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Hakika tunaona Mungu anavyozidi kumtumia mtumishi huyu wa Mungu kwa njia ya tofauti sana. Watu wengi sana wanafunguliwa katika vifungo vya shetani kwa maombi hatari anayoyafanya katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Kuna watu wanakuja kanisani wakiwa na mizigo mikubwa ya mateso na taabu lakini wanapokutana na nguvu za Mungu kupitia mtumishi Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay na wachungaji wote wa Mlima wa Moto Mikocheni "B", mizigo yao inaondolewa na wanawekwa huru. Wapo waliokuja hapa kanisani wakiwa na kilio cha kupata watoto, kutozaa, mafanikio, magonjwa, roho chafu, ndoto chafu, kufukuzwa kazi, kutopata kazi, kudaiwa, kulogwa, kutumikishwa bila malipo, kukosa ada na kodi ya nyumba, kukosa mume/mke wa kuoa au kuolewa na mengine kama hayo lakini walipokanyaga hekalu la Mungu la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kukutana na nguvu za Mungu mateso yao yakafutwa na sasa wanafurahia uwepo wa Mungu katika maisha yako.

UJUMBE WA KUINUA IMANI YAKO KUTOKA KATIKA KITABU CHA MITHALI 10:

// 3. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumuia mbali.//

// 4. Atendae mambo kwa mikono mlegevu huwa masikini; Bali mkono wake mwenye bidii hutajirisha.//

// 6. Baraka humkalia mwenye haki kichwani; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.//

Tunatumaini ujumbe huu utafanya kitu katika maisha yako kama utausoma na kuufanyia kazi. BWANA anakuwazia mema kila kuitwapo leo, ni wewe kuamua kumtumikia kwa mali zako, ngu zako, elimu yako na maarifa yako. Unapojitoa kwa kazi ya Mungu bila kuangalia maslahi ndipo Mungu anakuandalia hazina yako hapo baadae. fanya kazi ya Mungu kama mtumwa ipo siku utaishi kama mfalme.

Jitume katika kazi yako, naye BWANA ataweka mkono wake juu ya kazi yako na itabarikiwa sana.

Ishi maisha ya imani na ya kumtegemea Mungu wakati wa shida na raha. Unapokumbwa na baya lolote lile usimkufuru Mungu wako bali mshukukuru kwa kila jambo, na umuombe akuepushe na mabaya katika maisha yako.

Mungu anatamani kuona nafsi ya mtu wake aifi njaa bali anatamani kila wakati nnafsi yako imeshibishwa. Haya yote yatafanyika kwakoa pale uutakapomkubali BWAN kuwa ni mwokozi wa maisha yako na kuyafanya yale yote akuagizayo kupitia watumishi wake au kwa kusoma Neno la Mungu katika Biblia.

Kwahiyo ukitaka kufanikiwa kimwili unatakiwa kufanya kazi kwa bidii na sio kwa ulegevu ili hapo baadae uwe tajiri kama Biblia inavyosema katika Mitahli 10:4. Juhudi zako ndizo zitafanya ufanikiwe na kuwa mtu maarufu na tajiri. Mungu wetu ataibariki kazi ya mikono yako, sasa kama huna kazi Mungu hataibariki mikono yako kwasababu hata akiibariki itafanya nini wakati hauna hata kazi. Muombe sana Mungu akupe wazo la kugundua kazi ya kufanya katika maisha yako ili aweze kuibariki.

Yawezekana unapitia changamoto fulani katika maisha yako, na umehangaika bila majibu, nataka nikuambie yupo Yesu mtenda miujiza na ishara, atafanya na kwako kama alivyofanya kwa wengine. Usikate tamaa bali endelea kufika kanisani, kuomba na kufunga, kutenda mema, kusoma Neno la Mungu na kulifanyia kazi, kunyeyekea, kuwa mtoaji kanisani, kuwaheshimu na kuwatii watumishi wa Mungu, onyesha upendo kwa kila mtu, kuzishika amri za Mungu na kuzifanyia kazi katika maisha yako na mengine kama hayo.

Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usaufiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni. Njoo na rafiki yako au ndugu yako. Mungu akubariki sana.
Mch. Noah Lukumay (Mch. Kiongozi) wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"




 Mch. Sylvanuus Komba wa kanisa la Mlima wa Moto Sabasaba Dodoma na mke wake


























 














Comments