29.09.2017: MWALIMU WA UCHUMI MARY NGOWI AFUNDISHA MAMBO MATANO YA KUZINGATIA UNAVYOFANYA BIASHARA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI (WOCA)

Mwalimu MaryNgowi siku ya Ijumaa 29.09.2017 aliweza kufundisha MAMBO MATANO (5) YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFANYA BIASHARA katika Kongamano la Wanawake na Uchumi la Kukomesha Kilio Cha Mwanamke. Kongamano hili limeandaliwa bure na Chama Cha Women For Christ Alliance (WOCA) cha Mlima wa Moto Mikocheni "B" chini ya Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, na siku ya Jumapili 01.10.2017 itakuwa ni hitimisho la kongamano hili ambalo litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Siku ya leo kongamano linaendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 mchana hadi saa 1 usiku. Walimu kama vile Mary Ngowi, Mch. Esther Mukasa, Mch. Dkt. Peter Mitimingi na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare watakuwepo kukufundisha masomo mbalimbali ya kiuchumi, kiafya, kiihuduma na mabo ya kifamilia. Pia siku ya Jumapili watakuwepo kukufundisha kwahiyoi ni siku yako wewe mwanamke kuamka na kuanza safari nyingine ya mafanikio.

Usafiri wa kufika kanisani utatolewa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Ukifika hapo utasikia watu wakisema kanisani kwa mama. au unaweza kuja kwa usafiri wako ili kuwahi mafundisho.


Mr Samweli Hillary (kulia) akiongea jambo na Mwalimu Mary Ngowi kabla hajaanza kufundisha somo la uchumi.
































ANGALIA VIDEO HII







Comments