29.09.2017: KIONGOZI WA CHAMA CHA WOMEN FOR CHRIST ALLIANCE (WOCA) ALIVYOHIMIZA WATU KUFANYA KAZI

Mama Mch. Noah Lukumay, kiongozi wa chama Cha Women Aliance (WOCA) - Mithili 31:29 chini ya Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, siku ya Ijumaa 29.09.2017 aliweza kuwatia moyo wanawake wanaotaka kufanya biashara. Alisema mtu anayetaka kufanya biashara ni lazima ajitambua, aangalie masoko, aangalie wateja wake wanataka nini, afanye kazi kwa wakati, atatue changamoto katika kazi, asikate tamaa, afanye kwa bidii, biashara anayofanya ifananie na yeye, kwa mfano kama mtu anauza wigi basi au nguo basi avae nguo kali za kupendeza au wigi zuri ili awe kivutio kwa mteja wake. Ni mambo mengi sana alitufundisha.

Kongamano hili lilikuwa la siku 8 na Jumapili 01.10.2019 litahitimishwa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuanzia saa 3 asubuhi hadi 8 mchana.

Walimu watakaofundisha siku hiyo ni Mch. dr. Peter Mitimingi, Esther Mukasa, mary Ngowi na wengine wengi. Na siku ya Jumamosi 30,09.2017 kutakuwa na kongamano kuanzia saa 9 mchana hadi saa 1 usiku.

Kwa siku 6 zilizopita watu wengi sana wamepokea majibu yao kupitia mafundisho ya Kukomesha Kilio Cha Mwananmke Kiuchumi.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

Mama Mch. Noah Lukumay









Comments