25.09.2017: MAFUNDISHO YA MCH. PETER MITIMINGI KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI LA KUKOMESHA KILIO CHA MWANAMKE

WATU WA KWANZA KUCHANGAMKIA MAMBO MBALI MBALI NI WANAWAKE!

1. Asilimia kubwa ya watu wa kwanza kufika ibadani kanisani ni wanawake.

2. Ukichunguza watu wa kwanza kuitikia mambo huwa ni wanawake,

• Kama ni Kufunga na kuomba

• Kama ni kujitolea sadakaau vitu

• Kama ni kutubu n.k


ASILIMIA KUBWA YA WATU WALIO SUPPORT HUDUMA YA BWANA YESU KIFEDHA WALIKUWA WANAWAKE

1. Wanawake ndio waliokuwa mstari wa mbele kusupport huduma ya Yesu hata kifedha - Mariam Magdarena, Joanna - Yule aliyetolewa pepo wachafu, Susana Luka 8:2-3, Luke 24:10.

2. Wanawake ndio walimfuatilia Yesu hadi mwisho mpaka anauwawa. Yohana 19:25

3. Wanawake ndio waliokuwa wa kwanza kuwahi kuliangalia kaburi la Yesu. - Yohana 20:1-2

4. Wanawake ndio waliokuwa wa kwanza kujua kwamba Yesu amefufuka na kwamba hayupo tena Kaburini.


UMUHIMU WA NAFASI YA MWANAMKE

1. Utafiti umebaini kuwa Wanaohimiza ibada za majumbani ni mwanamke.

2. Wanaohimiza watoto kwenda kanisani ni mwanamke.

3. Wanao kagua madaftari na maendeleo ya watoto ni wanawake.

4. Wananwake ndio huwa watu wa kwanza kumuona adui anapoingia katika familia. Mwanamke alikuwa wa kwanza kumuona adui pale bustanini Mwanzo 3: 2-3


NI NANI AMBAYE HAKUSAIDIWA NA MWANAMKE

Katika utafiti (research) uliohusisha watu elfu kumi, (10,000) waliulizwa swali kwamba ni mtu gani aliyekushawishi zaidi katika mambo ya Mungu na kiimani katika maisha yako?

Walliowengi walisema ni mama yangu.

Wanaume weliooa walisema mke wangu.



































































Comments