24.09.2017: WAGENI, WACHUNGAJI, WAZEE WA KANISANI, WALIMU WAKIWA KATIKA OFISI YA MH. BISHOP DR. GERTRUDE

TAFAKARI UJUMBE HUU:

// Unapotaka kujiingiza katika masuala yatakayokunufaisha, ni lazima ujifunze kuutumia vizuri wakati wako kama unavyozitumia vizuri fedha zak

// Weka malengo iwapo unataka kuutumia muda wako vizuri. Weka ratiba inayoonyesha malengo na shughuli zako nyingine. Andika kila shughuli utakayoifanya siku hiyo na hata siku inayofuata.//

// kwa kupanga vyema shughuli zako za kila siku ni dhahiri kila wiki na kila mwaka wako moja kwa moja vitajipanga.//

// Waajiriwa lazima wajifunze kuongeza vipato vyao kwa kufanya kazi za ujasiriamali baada ya kuondoka kazini.//

Baada ya kupata masomo ya kujikwamua kutoka katika umaskini kutoka kwa walimu mbalimbali katika Kongamano la Wanawake na Uchumi la Kukomesha Kilio cha Mwanamke kinachotokana na maswala ya Kiuchumi, Kiafya, kifamilia, Kihuduma na Kifedha baadhi ya wazee wa kanisani, wageni, walimu, wachungaji na watumishi mbalimbali waliweza kufika katika ofisi ya Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na kuweza kubadilishana mawazo.

Kongamano hili linaloendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" mpaka tarehe 01.10.2017 ni kwa watu wote, dini zote makabila yote na hakuna kiingilio. Siku za katikati ya wiki linaaza saa 9 mchana hadi saa 1 usiku na siku ya Jumapili litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Waandaji wa kongamano hili ambao ni Women For Christ Alliance (WOCA) Mithali 31:29 wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wanakualika wewe mwanamke unahitaji maisha yako yawe bora kimwili na kiroho. walimu wamejipanga kuhakikisha unapokea kile ambacho Mungu alipanga kikufike na kifanyike baraka katika maisha yako.

WOCA chini ya Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wamekuaundalia walimu wengi sana ambao ni Mch. Peter Mitimingi, Mashauri, Esther Mukasa, Mary Ngowi na ma-bankers.

Mungu na akubariki sana..Usikose kabisa siku hizi 8 za kujikwamua katika UMASKINI.

Mch. Peter Mitimingi na mke wake wakibadilishana mawazo na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare


 kutoka kulia ni Mjasiriamali Mashauri, Samwel Hillary na mke wa Mashauri




Mwalimu Esther Mukasa

 Kijana wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" akiongea na Bishop


Rose Rwakatare (kushoto) akiongea na mama yake mzazi














 xxx













































Comments