24.09.2017: WAANDISHI WA HABARI WAKIONGEA NA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE JUU YA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI LINALOENDELEA MPAKA 01.10.2017

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alivyoongea na waandishi wa habari kuhusiana na Kongamano la Wanawake na Uchumi la kukomesha Kilio cha Mwanamke Kiuchumi, Kiafya, Kihuduma, Kifamilia na Kifedha. Kongamano hilo lilizinduliwa siku ya Jumapili 24.09.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Kongamano hilo linaendelea mpaka siku ya Jumapili 01.10.2017, siku za katikati ya wiki linaanza saa 9 mcaha hadi saa 1 usiku na ni kwa kila mtu bila kujali dini, dhehebu, kabila, rangi au taifa la mtu.

Kingamano hili lilihudhuria na maelfu ya watu waliokuja kupokea baraka zao kupiti watumishi wake walioandaliwa kwaajili ya kuwalisha watu chakula cha uzima maisha yao.

Wewe mwanamke unayepitia changamoto za maswala ya Kiuchumi, Kiafya, Kifamili, Kihuduma, usikose hizi siku 8 za kupokea majibu yako kutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake

Endelea kufuatilia post zetu wakati tunakuandalia kile alichokizungumza Bishop pamoja na waandishi wa habari.

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiongea na waandishi wa habari.
















Comments