24.09.2017: MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIHUBIRI SIKU YA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI

Wakati tupo katika maandalizi ya kuandaa somo alilofundisha Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare katika kongamano la Wanawake na Uchumi lililozinduliwa rasmi na Mh. Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 24.09.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", tumeona ni vyema ukaona matukio katika picha ya hili kongamano lililoandaliwa na chama cha Women For Christ Alliance (WOCA)-Mithali 31:29 chini ya mbemba maono wa kanisa la Mlima wa Moto Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Dhumini la kongamano hili ni kumuinua mwanamke Kiuchumi, kifamilia, kiafya na Kihuduma ili asonge mbele na kujitambua, kujithamini na kujiamini kuwa kama mwanamke anaweza kufanya lolote na kwa ukubwaaaa.

Kongamano linaendelea mpaka Jumapili 01.10.2017, na katikati ya wiki linaanza saa 9 mchana hadi saa 1 usiku. Hakuna kiingilio kabisa..

Watu wengi walifika pamoja na walimu mbalimbali waliweza kufundisha. Baadhi ya walimu ni Mch. Peter Mitimingi, Mjasiriamali Mashauri. Na siku ya leo na kuendelea watafundisha ikiwa ni pamoja na Mwalimu Esther Mukasa, Mary Ngowi na wengine wengi.

 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare












































































Comments