24.09.2017: MAMIA YA WATU WAOKOKA KATIKA KONAGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hivi ndivyo watu walivyomiminika katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakihitaji kuokoka. Hii ilitokea katika uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Uchumi la Kukomesha Kilio Cha Mwanamke siku ya Jumapili 24.09.2017. Mch. Francis Machichi aliongoza sala ya toba na wachungaji waliweza kuwaombea. Baada ya ibada kumalizika walipelekwa enero maalum kwaajili ya kubatizwa kwa maji mengi.

Kwako wewe unahitaji kuokoka nafasi bado ipo, tunakukaribisha katika kongamano hili linaloendelea mpaka siku ya Jumapili 01.10.2017 kuanzia saa 9 mchana hadi saa 1 usiku. Kwa siku hizi 8 utajifunza masomo ya kuinua uchumi katika maisha yako na wewe ambaye hujaokoka utaongozwa sala ya toba na kuombewa.

Kumbuka ya kuwa kongamano hili ni la dini zote, mataifa yote, makabila yote, rangi zote. Limeandaliwa kwaajili yako na bila kiingilio ili maisha yako yabadilike. Walimu na wachungaji wa Kongamano hili ni Mch. Mitimingi, Esther Mukasa, mary Ngowi, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na wengine wengi.

Unapokuja, unaombwa kuja na rafiki au jamaa yako ili naye apokee baraka hizi za mafanikio kutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake aliowaandaa kukupa ujumbe.

Siku ya Jumapili 01.10.2017 kongamano litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Karibuni nyooooteeeee.



































Comments