24.09.2017: KWAYA YA WOCA ILIVYOIMBA SIKU YA JUMAPILI KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mama Mch. Francis Machichi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kufanya maombi katika kongamano la Wanawake. Watu walibarikiwa sana na maombi kutoka kwa mtumishi wa Mungu kwasababu yalikuwa na kibali kutoka kwa Mungu. Mama huyu amefanyika baraka kubwa katika kanisani kwa matendo yake na jinsi anavyojituma kufanya kazi ya Mungu. 

Kongamano hili ambalo lilizinduliwa siku ya Jumapili 24.09.2017 linaendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" mpaka Jumapili 01.10.2017. Muda wa kuanza kongamano kwa siku za kazi ni saa 9 mchana hadi saa 1 usiku.Siku ya Jumapili litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Wewe mwanamke usikose kongamano hili kwani limeandaliwa kwaajili yako na jamii yako inayokuzunguka.

Mwanamke umeteseka sana kiuchumi lakini leo Mkombozi wako Yesu Kristo amekuandaliwa walimu malidadi watakao kupa maarifa ya kupata fedha na pia kupata mafundisho ya rohoni. 

baadhi ya walimu watakaofundisha ni Mch. Peter Mitimingi, Esther Mukasa, Mashauri, mary Ngowi. Kupitia watumishi hawa maisha yako yanakwenda kubadilika na kuwa bora zaidi. Unatakiwa kuzingatia utakachofundishwa na kukifanyia kazi.



















Comments