24.09.2017: KASAKI SELEMANI ALIVYOSHUSHA UWEPO WA MUNGU KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Kasaki Selemani siku ya Jumapili 24.09.2017 katika konagamano la Wanawake na Uchumi la Kukomesha kilio cha Mwanamke aligusa miyo ya watu kupitia nyimbo yake yenye mafuta ya BWANA. 

Kumbuka Kongamano jili limeandaliwa na Chama Cha Women For Christ Alliance (WOCA) cha wanawake wa Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Ni Kongamano la siku 8 na limeanza Jumapili 24.09. na litahitimishwa 01.10.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". katikati ya wiki kongamano linaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku, na siku ya Jumapili litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. 
walimu mbalimbali watakuwepo kwa siku hizo zote 8 kama vile Mary Ngowi, Mashauri, Mch. Peter Mitimingi, Esther Mukasa na wengine wengi. BWote mnakaribishwa




Comments