24.09.2017: KAMATI NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WOMEN FOR CHRIST ALLIANCE (WOCA) WALIVYOPIGA PICHA ZA KUMBUKUMBU

TAFAKARI HUU UJUMBE
//Mafanikio hayawezi kupatikana bila ya nidhamu katika matumizi ya wakati.//

//Watu wenye mafanikio hufanya kazi muda mrefu zaidi kuliko watu wasio na mafanikio.//


// Ukitaka kufanikiwa kifedha, huna budi kuwa na mipango ya kuingiza fedha mchana na usiku.//

Ewe mwanamke unahitaji kufanikiwa kiuchumi, unakaribishwa katika kongamano la wanawake na Uchumi la Kukomesha Kilio cha Mwanamke linaloendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" mpaha tarehe 01.10.2017. Kongamano hili linaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku kwa siku 8. 

Siku ya Jumapili 24.09.2017 ilikuwa ni siku ya kwanza ya uzinduzi wa kongamano hili la Mwanamke na Uchumi la Kukomesha Kilio Cha Mwanamke ambalo limeandaliwa na Chama Cha Women For Chrst Alliance (WOCA)- Mithali 31:29 cha Mlima wa Moto Mikocheni "B" chini ya Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare..

Baada ya kupata masomo na mahubiri kutoka wa wageni waalikwa Mch. Peter Mitimingi na Mjasiriamali aliyefanikiwa Bw. Mashauri; kamati , viongozi na wajumbe wa WOCA walliweza kupiga picha ya kumbukumbu kama unavyoona katika picha hapo chini.

Siku ya Jumapili 01,01.2017 kongamano litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana, kwahiyo wahi mapema ili upate nafasi yako. Watu ni wengi sana wanaofika katika kongamano hili kwa siku za katikati ya wiki. 

Kupitia kongamano hili ninaamini Mungu atafungua milango katika maisha yako na utakwenda kufanikiwa. Unachotakiwa ni kuyafanyia kazi yale yote unayofundishwa Usiwe ni mtu wa kusikiliza na kupuuzia. Maamuzi yako na jitihada zako ndizo zitafanikisha lengo lako na kufikia pale unapotaka kupafikia. Pia mshirikishe Mungu kwa kila hatua unayochukua katika kazi yako ili naye ahusike katika safari yako ya mafanikio.

Mungu akubariki sana na karibu katika kongamano la Wananwake na UCHUMI




















Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa na walimu 

















 


































Comments