24.04.2017: KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI LA KUKOMESHA KILIO CHA MWANAMKE MISAADA YATOLEWA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Katika Kongamano la Wanawake na Uchumi la Kukomesha Kilio Cha Mwanamke lililoandaliwa na chama cha Women For Christ Alliance (WOCA) - Mithali 31:29 cha kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", waliweza kutoa misaada kwa yatima, wajane kama vile mchele na uniform.

Kongamano hili lilizinduliwa rasmi na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 24.09.2017 na litahitimishwa siku ya 01.10.2017 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Katika kongamano hili kutakuwa na walimu mbalimbali kama Mch. Peter Mitimingi, Esther Mukasa, Mary Ngowi, Mashauri na watu wa mabenki watatoa masomo mbalimbali. Muda wa kuanza kwa siku za katikati ya wiki ni saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku.

WOCA tunakualika wewe mwanamke unahitaji kukombolewa kiuchumi, kifaya, kihuduma kwa siku 8 ili uweze kukutana na muujiza wako wa mafanikio kupitia watumishi wa Mungu.























































































































































































Comments