27.08.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AFANYA MAOMBI MAALUM KATIKA TAMASHA LA MAOMBEZI -

Zipo faida nyingi sana kama utaamua kuwa mtu wa maombi. Unapoomba ndipo BWANA anafanya kitu katika maisha yako kulingana na maombi yako. Jijengee tabia ya KUOMBA kila kuitwapo leo..

Mh. Dr. Gertrude Rwakatare akishirikina na jopo la wachungaji na watu wote waliofika katika ibada ya Tamasha la Maombezi lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 27.08.2018 waliweza kufanya maombi maalum ili Mungu aweze kutuokoa katika milango iliyofungwa na maadui zetu tusisonge mbele kimaendeleo na kuimarisha imani zetu.

Watu wengi sana wanapitia changamoto katika kazi zao, ndoa zao, afya zao, biashara zao, safari zao, mashamba yao, mifugo yao, mahusiano yao, masomo yao na wengine wametupiwa majini na mapepo, wanaota ndoto chafu, wanasengenywa, wanakatishwa tamaa, wanadaiwa, wanafukuzwa kazi, waondolewa vyombo katika nyumba zao za kupanga kwa kukosa kodi, wamefungwa na nguvu za giza na kila wanalofanya halifanikiwi n.k. Kutokana na hayo, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alipata maono ya kufanya tamasha la MAOMBEZI ili kila mtu aombe kulingana na changamoto anazopitia. Pia aliweza kuwaombea watu wote ili Mungu awafungue katika mitego ya shetani. Tunamshukuru sana Mungu kwani walio wengi walifunguliwa kutoka katika mateso ya adui shetani.

Ninachotaka kukuambia ndugu yangu, wewe mshike huyu Yesu na ufanye yale anayokuagiza kupitia watumishi wake na kusoma sana Neno la Mungu. Unaposoma Neno la Mungu ndipo unapopata mwanga wa kujua siri za Mungu na njia za kupambana na maadui zao. Wapo watu wengi sana walikuwa wanapitia magumu lakini walipoamua kuwa na huyu Yesu na kutii yale anayowaagiza, Mungu aliweza kufungua milango ya mafanikio na sasa wanafurahia wokovu wao. Pia jitahidi za kufanya maombi na kufunga kula chakula ili kuutiisha mwili wako

Zipo faida nyingi sana za kufunga na kuomba.

1 Imani yako inaoongezeka i.
Mathayo 17:21 ‘’ [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] ‘’

2. Kupitia macho yako ya ndani unaweza kuona yaliombele yako na unaweza kupata njia za kuepukana nayo.
Zaburi 119:18 ‘’ Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. ‘’

3. Mwili wako unatiishwa. Unapotiisha mwili wako inakusaidia kuepukana na dhambi.
Wakolosai 3:5 ‘’ Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;‘’

4. Unapokea kile ulichoomba maana ni ahadi ya Mungu.
Yeremia 29:13 ‘’Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.'' Tena Biblia inasema ''Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;-Mathayo 7:7'' na kwa sababu MUNGU analiangalia neno lake alitimize basi hata aliposema tuombe ni hakika atajibu maana yeye hajipingi na Neno lake, labda tu sisi tuombe vibaya na tupungukiwe na imani katika maombi yetu.
1 Yohana 5:14-15 ''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.''

5. Unampa nafasi Roho Mtakatifu kuwa pamoja na wewe na kukutumia.
1 Kor 12:11 ‘’ lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. ‘’

6. Unapata nguvu za kumtumikia Mungu..
Mathayo 11:12 ‘’Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.‘’

Zipo faida nyingi sana lakini leo ngoja nikupe hizi chache. Kwahiyo wale waliioomba kwa Roho wa kweli siku ya JUmapili, basi wategemee kupata faida hizo hapo juu na zingine nyingi ambazo hatukupata muda wa kuziandika.

Cha msingi ni wewe kuwa karibu sana Mungu, kusoma Neno lake, kuwa na upendo, kusaidia wenye uhitaji, kuishi maisha matakatifu, kuungama dhambi zako, kushiriki ibada mbalimbali, kuwa mtoaji kanisani, kutangaza Injili kwa kila mtu na mengine kama hayo.

Mwisho, nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Usafiri ni bure kwenda kanisani na kurudi kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, utasikia watu wakisema kanisa kwa mama Rwakatare


Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare



Mch. Noah Lukumay




























































Comments