20.08.2017: MCHUNGAJI KUTOKA CONGO AHUBIRI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 20.08.2017 Mchungaji kutoka Congo aliweza kushiriki ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" ya KUFUNGULIWA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZET ILI TUSIFANIKIWE na alikuwa na haya ya kusema, BWANA Yesu asifiwe, mimi hapo zamani nikiwa Dar es Salaam nilikuwa Mchungaji lakini sasa ni Askofu na ninaitwa MC. Mpagala nipo Kinshaza Kongo na ninaishi huko. Ninakumbuka madhabahu ya mwisho kuhubiri kabla ya kwenda Congo ilikuwa ni madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ninamshukuru Mungu kwa miaka kumi niliyofanya kazi ya BWANA kuna mambo mengi sana yalifanyika na kukawa na mabadiliko makubwa katika huduma yangu. Katika maisha kunaweza kuwa Mabadiliko "Negative" au "Positive" na ndio maana nilipokuja Dar es Salaam asilimia kubwa nimeona kuna mabadiliko makubwa sana ambayo ni positive, kwa mfano nimeona kuna mabasi ya mwendokasi ambayo sijawahi kuona, pia majengo makubwa makuba. Pia nimeshangaa kuona kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" limekuwa kubwa sana tofauti na nilipokuwepo kipindi cha mwanzo., watu ni wengi na wenye hofu ya Mungu.

naomba nikupe Neno la Mungu lililosawa na "Mlima". Unajua katika katika kitabu cha Obadia 1:17 katika kile kipindi cha zamani cha watumwa, tunaona watumwa walikuwa wanachukuliwa Afrika na kupelekwa sehemu mbalimbali, na watumwa wengi hawakuweza kujikomboa bali wengi wao wamekufa katika hali ya utumwa wakiwa maskini na fukara. Lakini kuna watu wachache waliweza kujikomboa kwa mfumo fulani na fikra fulani. Kitu walichotumia kujikomboa ni kutumia silaha hata kama wazungu walikuwa wana na kila kitu, na njia nyingine waliweza kukimbia kwenye milima na kupanda juu ya milima wakijua ya kwamba hata maadui zao wakija wataweza kuachia mawe ili yawabonde.

Na ndio maana katika Biblia inasema, "Katika Mlima Sayuni kutakuwepo wenye kuokoka, ambao kwa sasa ni wana Mlima wa Moto Mikocheni "B". Na watumwa wa Yakobo watamiliki milko zao na Yakobo atakuwa moto. Kuna baraka aina tatu za Mlimani nazo ni:-
1. Watu wa mlimani lazima wawe wamekombolewa (walio chini watakuwa juu)
2.Watu waliojuu ya milima lazima wamiliki milki yao, yaani cha kwako hakuna atakayekipokonya kwasababu ni chako kutoka kwa Mungu.
3. Utakuwa moto katika Jina la Yesu Kristo.


Bwana akubariki na kukutendea mema..Amen
















Comments