20.08.2017: MAMIA YA WATU WAOKOKA KATIKA IBADA YA KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU KATIKA MAISHA YETU ILIYOFANYWA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"
Mlima wa Moto, Mlima wa
Moto Mikocheni “B”, Mountain of Fire, Mountain of Fire Tanzania, Mama Gertrude
Rwakatare, Mch. Gertrude Rwakatare, Askofu Gertrude Rwakatare, Mh. Bishop Dr.
Gertrude Rwakatare, Mlima wa Moto Tv, Rumafrica,Rumafrica online Tv, Rulea
Sanga, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Getrude Lwakatare, Gertrude
Lwakatale, Lwakatare, Mch. Getrude Lwakatare
Tuna kila sababu ya
kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya katika kanisa la Mlima wa Moto
Mikocheni "B". Siku ya Jumapili 20.08.2017 katika ibada ya
"KUFUNGUA MILANGO AMBAYO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU KATIKA MAISHA YETU ILI
TUSIFANIKIWE" watu wengi sana walijitokeza madhabahuni kwaajili ya
KUOKOKA. Mch. Noah Lukumay na Mch. Francis Machichi waliwaoongoza sala ya toba,
waliwaombea na baada ya ibada kumalizika wainjilisti na wachungaji mbalimbali
waliwabatiza kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku yao ya
kujifunza masomo ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni
"B" kuanzia saa 9 alasiri.
Ndugu yangu wewe ambaye
hujabatizwa na kuongozwa sala ya toba, Mungu anakuhitaji, anatamani kukuona
unaishi maisha matakatifu ili siku ya mwisho ya kuishi hapa duniani ukaonane
naye huko mbinguni. Unatakiwa kutambua kuwa hujui kesho yako, anayejua ni Mungu
wako, hujui baya gani litakukumba baada ya kuondoka hapo ulipo, unatakiwa
kujiuliza kuwa baada ya maisha ya hapa duniani nini kitafuata? Sauti ya Mungu
inakuita sasa...OKOKA na umtumikie Mungu.
Pengine unatamani kuokoka,
tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8
mchana. Watumishi wa Mungu wakiongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
wanatakuombea na kukuongoza sala ya toba na utabatizwa kwa maji mengi siku hiyo
hiyo. Mungu akubariki sana..
Tunakukaribisha katika
ibada ya Jumatano saa 9 alasiri, Ijumaa saa 9 alasiri na Jumapili saa 3 asubuhi
hadi saa 8 mchana. Siku ya Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi
cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, na baada ya ibada
utarudishwa kituoni. Njoo na rafiki yako.
Mch. Noah Lukumay akiwaongoza sala ya toba na kuwaombea waongofu wapya.
Comments
Post a Comment